Nifah
JF-Expert Member
- Feb 12, 2014
- 34,020
- 79,098
Unajua wakati mwingine uzoefu wa maisha usipokuwa makini waweza kukufnya uonekane kuwa punguani hasa hasa maeneo ya watu waliostaarabika.
Katika JF ukikuta ID ni ya zamani mfano 2006 unatarajia kupata maoni yenye busara, maana inasemwa kuwa waliokuwepo wakati wa Jambo forum walikuwa wanashusha pweiti za kutosha za kuwa zindua watanzania kutoka fikra mgando kwa staha ya hali ya juu. Lakini inashangaza sana NN mbali na uzoefu wote huu wa kushiriki hapa JF (posts 49 961) bado anaendelea kubadilika kifikra kutoka mbaya kwenda mbaya sana hasa linapokuja suala la utumiaji wa lugha ya kiuungwana.
Ndiyo maana nasema uzoefu wa maisha ya maeneo fulani unaweza kukufanya uonekane punguani maeneo mengine. Eneo analoishi NN linaweza kuwa na mchango mkubwa kwenye kuharibu uwasilishaji wa kistaarabu wa hoja zake hapa JF.
Umeongea kitu cha maana sana.Ngoja ninyamaze nisijepigwa 'mawe' mie!