Ponjoro
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 442
- 396
Kumekuwa na malalamiko ya wasanii wengi kulalamika kuibiwa nyimbo zao na msanii diamond platinum, alivyotoa "mbagala" kuna bwamdogo aliyeimba "tandale " alilalamika kuibiwa hiyo nyimbo,alivyotoa kibao cha nataka kulewa hbaba alikuja juu na kulalamika kuibiwa nyimbo yake na sasa hiki kibao kipya cha my number 1 nacho kimezidi kuleta tabu ambapo dayna anadai beat kaibiwa na baba levo ambaye bila shaka wote ni wa kigoma maana walifanya ngoma ya kuusifu mkoa wao hawa pamoja, naye anakuja juu kulalamika kuibiwa nyimbo na huyu kijana.kwanini wasanii wote hawa wamsingizie yeye? Maana isije kuwa kukubalika kwake ndiyo kunafanya watu wasiamini hata kama akiwa ni mwizi maana "apendwaye hulindwa" by the way kazi zake ni nzuri...