Nadhani ulichofanya hapo ni kuchukua hao waliokufa katika mazingira ya namna hiyo kwa kuwahusisha na taaluma zao, wapo watu wa kada mbalimbali kama walimu, madaktari, wanasheria, wasiokuwa na taaluma yoyote, vichaa, wanajeshi, wanasiasa, viongozi wa dini n.k ambao wamejiua au wamekufa katika mazingira ya namna hiyo ambao ukitaka kuwachambu wa taaluma au tabia zinazofanana over ages unaweza ukapata orodha ndefu zaidi ya hiyo. Kwa hiyo siamini kama ni watu wenye uwezo wa kitaaluma au elimu kama hao ndo wanajiua zaidi. Kujiua limekuwa ni tukio linalofanywa na binadamu wa aina zote.