Kwani ni uongo kuwa walimu ni maskini? Ni uongo kuwa walimu wanaishi maisha magumu?kama kusema hayo ni kuwadharau walimu basi walimu wa nchi ni maskini na wanaishi maisha magumu kwasababu ya kutokujitambua,kundi kubwa la walimu mishahara Yao hauzidi 150000 kwani wamekopa kwenye mabenki wafikia 1/3 inayotakiwa kisheria basi wameamua kwenda kulipa kwenye taasisi zisizozingatia Sheria Kwa kuwakopesha walimu Kwa mdhamana wa ATM card,mshahara ukitoka Wanaudraw ndipo kiasi kinachobaki wanamgawia mwl.je mwl huyu asiambie lolote Kwa kuogopa kuwa anadhaurika.
Jambo la msingi ni kupiga kelele Kwa watawala Ili waboreshe maslahi ya walimu,maslahi ya walimu ni kiduchu sana hawawezi kupiga hatua yoyote