Kwanini Watanzania hawapendi kusafiri?

Kwanini Watanzania hawapendi kusafiri?

Labda Nikuulize Mtu aliyekimbia kutoka Tanzania bila hati ya kusafiria Anakuambia alikimbia nini hapa Tanzania?
Nimebahatika kutembea kidogo
Let me tell you
Wenzetu wengi kwenye nchi zao ukitoa watalii Wanakimbia shida, Wachache wanaotafuta fursa.
Mtoa mada nikupe tu mfano hapo Kenya.
Kenya ukifanya mchezo unakufa Hata kula huli na hakuna mtu anakuonea huruma Na ni Raia wa pale. Kitu ambacho Tanzania hakipo
Nenda Canada Wakenya wamejaa huko wamekuwa chokoraa Barabarani lakini Hawataki kurudi nyumbani
Hadi Ndugu Wakenya walioko kule wanajichanga kuwanunulia mabranket na chakula ughaibuni
Si Bora ukae kwenu kama huna sababu ya kusafiri
Tanzania ni pazuri sana Laiti Serikali ingetengenezea fursa vijana wapambane
Kuliko kulifanya Taifa ni la watu flani tangu uhuru.
 
Watakwambia mambo ya vacation/ holiday ni ya wazungu [emoji3][emoji28]

Wazungu mambo mengi hufanya for reasons.
 
Iko hivi ukiangalia wazungu wengi ni watu ambao wanafanya sana saving hata wenye vipato vya kawaida.

Wanaweza saving kwakuwa kwanza kiwango cha utegemezi kwao ni kidogo sana. Yani utakuta baba na mama wana mtoto mmoja au hawana na hamna mtu anaewaomba hela.

Hakuna sijui michango ya ukoo, sijui mtoto wa mjomba ada shule, mara rafiki anaoa, mara bibi anaumwa n.k

Birth control imesaidia wenzetu sana. Sisi huku mtu ana ndugu zaidi ya laki na akipata tu ka ajira ka kulipwa laki saba basi kila mtu anamtolea macho, vizinga visivyoisha.

Huyo mtu ata save sangapi ili aweze kutembelea nchi mbalimbali?

Kingine kwa wenzetu wa nje huko wengi wanakula generational wealth. Yani mtu anazaliwa anakuta familia iko well-off kuanzia vizazi kadhaa vilivyopita. So yeye anaendeleza kutengeneza hela tu na future ya kizazi chake so mambo kama kusafiri ni kawaida tu.

Chamwisho ni nchi yetu hii ina mifumo ya ajabu sana. Mtu kumiliki passport tu inaonekana kama vile ni jambo la ajabu sana. Ukienda uhamiaji kutaka passport inakuwa ni mchakato mgumu utadhani unataka kwenda mbinguni.

Nchi za wenzetu kuwa na passport ni kawaida na kila raia anayo kama document muhimu. Hapa kwetu passport inachukuliwa tofauti sijui kwanini CCM hawataki raia wamiliki passport?
Yani inaonekana ulikua kipanga sana wa kuandika Essay...hongera ssna
umemaliza kila kitu
100%
 
Mwanamke aitwaye Cassandra de Pecol kutoka Connecticut, alifanikisha ndoto yake ya kutembelea nchi zote duniani, 193,
akiwa na umri wa miaka ishirini na saba.

Mpaka anafikisha miaka 18, Canada ndiyo nchi pekee aliyokuwa amefika, tena, ni kwa vile mama yake anatokea huko. Sababu kubwa iliyomfanya asisafiri akiwa mdogo ni uwezo mdogo wa kifedha.

Kufanikiwa kwake kuzitembelea nchi 193 ni jitihada zake binafsi. Anavyoonekana si tajiri, ila anapenda kusafiri. Lakini kuna Watanzania ambao pengine wana uwezo mkubwa kifedha kumzidi yeye lakini bado hawasafiri.

Ukizilinganisha nchi za Afrika Mashariki, hasa Kenya, Uganda, na Rwanda, Watanzania ndiyo wanaoongoza kwa kutokusafiri kwenda nchi zingine. Kwa nini hivyo?

1. Umaskini?

2. Lugha?

3. Ugumu wa upatikanaji wa passport?

4. Ushamba?

5. Utamaduni?

Sababu ni nini?
Namba 3 hasa ndo kipengele
 
Miaka fulani tuliendaga tel aviv
Huko tulikutana na watanzania waliyokaa muda mrefu sana huko
Kuna mzee mmoja huko alinikaribisha
Kwake somebody gasper matunda,aliniambia alipokuwa bongo
Alikuwa tanzania elimu supplies
Sema amejikita huko na yuko vzr alikuwa

Ova
Walikuwa na uraia wa Israeli?
 
Kwanza ukifanya simple survey kujua iwapo wabongo wanajua faida za kusafiri nina uhakika Kama wapo ni wachache sana 1 katika 100000.

Ndio maana wanakwambia hawawezi kusafiri bila sababu ya msingi [emoji3][emoji28]
Uko sahihi mkuu. Ndiyo maana wengine wanafikiri watu wanaopaswa kusafiri ni ambao nchi zao zina matatizo.
 
Back
Top Bottom