Kwanini Watanzania hawatumii aina hii ya matofari?

jiwe angavu

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2015
Posts
20,419
Reaction score
39,217
Wakuu habari.

Tumezoea kuona maeneo mengi nchini wakitumia aina mbalimbali za matofari katika shughuli nzima za ujenzi..kuanzia matofari ya tope yale ya kuchoma na pia matofari ya simenti au kwakizungu ni cement building blocks.

Katika haya matofari ya simenti tumezoa haya ambayo ni tofari ambalo linameungana lote.

Haya matofari yanakula sana mchanga na simenti pia yanahitaji maji mengi sana kuyamwagilia ili yaweze kua imara...kingine matofari haya ni mazito sana. Pamoja na sifa hizo bado yanaendelea kutumika maeneo mengi nchini.

Je, kwanini hatutumii matofari haya ambayo kwanza yatumia simenti na mchanga kidogo pia maji sio mengi yanayohitajika na pia yana uzito mdogo kurahisiha ubebaji na usafirishaji wake.

Je, ni kwasababu zipi zinachangia aina ya matofari haya yasitumike hapa nchini.

Picha nimeambatanisha[emoji116][emoji116][emoji116]

#MaendeleoHayanaChama

 
Sina uzoefu nayo sana ila nadhani hayo yanahitaji cement nyingi ili yawe imara kutokana na kua na nafasi kwa kati kati sasa hizi karakana zetu za kuzalisha matofali kwa mwendo wao wa mfuko mmoja kwa tofali 40 siyatakua yanabomoka hata kwa kuyatikisa tu ?!
 
 
Je, ni kwasababu zipi zinachangia aina ya matofari haya yasitumike hapa nchini.
Nahisi labda uhitaji wake kwa maeneo yetu, hatuhangaiki sana kuendesha joto ndani ya nyumba. Lipo wastani automatically nje na ndani sio tofauti ya kutisha, au simply we dont care.

Hiyo ni kama kweli yapo namna hiyo kwa ajili ya kucontrol joto🤦‍♂️
 
Ndugu yangu aliyatumia haya katika ujenzi maeneo ya Lugalo, sasa hivi nyumba yote ina nyufa.
Kwamba yanasababisha kuleta nyufa au?naomba logic ya uhusiano wa aina hiyo ya matofari na nyufa katika nyumba.

Je haya tunayotumia sasa huwa hayaleti nyufa katika nyumba?

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukienda Njombe Kuna sehemu inaitwa Imiliwaha Kuna Convent kubwa sana ya masista wa kanisa Katoliki. Wamejenga kamji kao.. Wanatumia hizo Tofali miaka na miaka.

Nadhani ni suala la mazoea na uelewa. Mf. Arusha wanatengeneza Tofali sijui wanatumia moram au nini ila ni ngumu sana.. Hata Kenya wanatumia hizo kama Arusha. Na huwa hawapigi plasta nje.
 
Panya Road,hizo hollow blocks hazifai
 
Tofali hizi hazina nguvu ya kubeba mzigo juu yake, hivyo hutumika zaidi katika kuta za ndani ambazo hazibebi uzito wowote zaidi ya kutenganisha vyumba.

Zaidi zina tabia ya kupenyeza maji.... kwa tabia hii hazifai kwa kuta za nje.
 
Tofali hizi hazina nguvu ya kubeba mzigo juu yake, hivyo hutumika zaidi katika kuta za ndani ambazo hazibebi uzito wowote zaidi ya kutenganisha vyumba.

Zaidi zina tabia ya kupenyeza maji.... kwa tabia hii hazifai kwa kuta za nje.
Lakini si kuna linta..pia mbona maeneo mengine yanatumia vzr tu kwa kuta za nje.

#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…