Kwanini Watanzania hawatumii aina hii ya matofari?

Katika uwekaji wa cement ili kupata ratio sahihi, inabidi mafundi wasimamiwe kwa mtutu wa bunduki.
Hili ni tatizo kubwa sana..nchi hii kila mtu mpigaji.

#MaendeleoHayanaChama
 
Lakini si kuna linta..pia mbona maeneo mengine yanatumia vzr tu kwa kuta za nje.

#MaendeleoHayanaChama
Ukitumia kama kuta ya nje inabidi kujua kuwa ukuta huo sio imara na ujiandae kwa matengezezo ya mara kwa mara....

Kumbuka tu aina hii ya matofali ni kwa ajili ya partition wall
 
Upo sahihi hayo matofali yapo wazi katikati ili kufanya insulation na yapo ya aina nyingi ya hivyo, kuna mengine ya kuchoma lakini nayo yanakuwa na uwazi pia.

Mimi nimeona yakitumika katika nchi yenye joto sana.

Sio hivyo hata namna ya ujenzi pia ni tofauti na kwetu, unakuta wanajenga kwa kuweka kuta mbili (double walling) na kuacha uwazi katikati, hivyo ukuta unakuwa mnene wenye uwazi kati, yote lengo ni hilohilo kufanya insulation ili kuzuia joto kuingia ndani kirahisi.
 
Hizo ni concrete bricks, huwa zinatengenezwa kwa na zege lenye simenti ya kutosha, pamoja huo awazi kati lakini zinakuwa imara sana.
 
Asante kwa ku verify
 
Hizo ni concrete bricks, huwa zinatengenezwa kwa na zege lenye simenti ya kutosha, pamoja huo awazi kati lakini zinakuwa imara sana.
Uimara wa zege ni nondo... Je hizo zina nondo?
 
Kwenye huu uzi ni jirani yako huu ni ndugu yako tukueleweje?
Ndugu yangu aliyatumia haya katika ujenzi maeneo ya Lugalo, sasa hivi nyumba yote ina nyufa.
 
Nina uzoefu wa hollow blocks kwa sababu tulikuwa tunazitengeneza na kuzitumia kwenye baadhi ya miradi yetu.

1. Hollow blocks kwa hapa Tanzania ni bei ghali kuliko solid blocks, ndio maana ilitupelekea kuagize mashine ili tutengeneze wenyewe kuliko kuzinunua.
2. Mixing ratio ya hollow blocks ni ya kibabe ukilinganisha na solid blocks. Maana kuipata 7n/mm2 kwenye hollow blocks tulikuwa tunatumia saruji nyingi saana.
3. Hollow blocks Ni mepesi ukilinganisha na solid blocks, kwa hiyo hupunguza uzito wa jengo. Ndio maana tunashauri zaidi yatumike katika framed structure na kwenye kuta za ndani za majengo ya load bearing walls

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi nilimeziona sana monduli ni nyepesi sana ila ni ngumu hatari,

Sent from my SM-S920L using JamiiForums mobile app
 
Ndugu yangu aliyatumia haya katika ujenzi maeneo ya Lugalo, sasa hivi nyumba yote ina nyufa.
Niliyakuta Mafinga huko Iringa, mchina anayazalisha na kujengea kiwanda chake. Karibu nusu ya uzalishaji wake inapasuka kabla ya kutumika.
 
Arusha ratio yao ni moram, dust, mchanga kidogo na cement. Tofali yao heavy utaipenda. Japo wanaozalisha hizo hollow blocks pia sio wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…