Kwanini Watanzania tunajenga utamaduni wa kubanana?

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Watanzania tuna utamaduni wa kubanana sana. Ukiingia kwenye daladala, hakuna mtu atakayefanya jitihada za kutobanana, utakuta abiria anamwegemea abiria mwingine bila kupata ridhaa mradi tu "sote tubababe."

Konda wa daladala anaweza kujaza abiria kuliko uwezo wa gari na kuwaacha wabanane na wala abiria hao hawawezi kulalamika.

Kwenye ujenzi wa makazi, utaona watu wanajenga mpaka kwenye mpaka wa kiwanja bila kuweka ile futi sita clearance kiasi kuwa mtu hawezi kupita katikakati ya viwanja viwili. Sababu yake ni nini?
 
Ni tabia inayokera sana ndani ya jamii, hawa makonda na madereva wao ipo siku watapigwa makofi na abiria wasiopenda kubanananishwa. Kuhusu kujenga mpaka mpakani bila kuacha nafasi nako ni kero na ujinga, unakuta jirani anajenga mpaka ukutani mwa jirani mwenzake ikitokea janga la moto hasara inaingia mpaka kwa mwenzake. Pia kuna kuambukizana wadudu na wanyama wasumbufu kama kunguni, chawa, papasi, mbu, utitiri, viroboto na panya. Sheria kali za ujenzi ziwepo ili kuzuwia nyumba kubanana
 
Hayo yote tisa, kumi uwe unasafiri na dada yako au mkeo.........heeeee, yataka moyo kuona kawaida 'kumbatio' analoweza kukutana nalo!!
 
Watanzania tuna utamaduni wa kubanana sana. Ukiingia kwenye daladala, hakuna mtu atakayefanya jitihida za kutobanana, utakuta abiria anamwegemea abiria mwingine kila kupata ridhaa mradi tu "sote tubababe."

Konda wa daladala anaweza kujaza abiria kuliko uwezo wa gari na kuwaacha wabanane na wala abiria hao hawawezi kulalamika.

Kwenye ujenzi wa makazi, utaona watu wanajenga mpaka kwenye mpaka wa kiwanja bila kuweka ile futi sita clearance kiasi kuwa mtu hawezi kupita katikakati ya viwanja viwili. Sababu yake ni nini?
Mimi ni mtu mbinafsi sana.
Ikiwa italazimika kupanda daladala au basi huwa sipandi iliyojaa vinginevyo mazingira yanilazimishe.

Kuhusu ujenzi.
Kiwanja cha kubanana hapana, niko tayari ninunue nje ya mji na nikijenga lazima niweke fensi.

Sipendi mikusanyiko kama sokoni au minadani, ile unapita ubavu ubavu kwsngu siko huru.

Kukaa vijiweni nako siwezi.
Nikimaliza kazi zangu huyoo nyumbani.
Kama sina ishu muhimu town sitoki.

Out zangu nyingi ni sehemu tulivu kwa njini, nje ya mji, milimani, waterfalks na mbugani...hopo roho yangu huburudika....

Nahisi mimi mbinafsi sana
 
Wewe sio Mbinafsi unapenda nature na utulivu, mimi pia next time tualikane mbugani na waterfalls,
Milimani hapana, nina phobia ya height (acrophobia) 🥲
 
Hiyo ya ujenzi wa makazi kuna mtu kanikomesha hadi nyumba yenyewe imenitumbukia nyongo, yaan namchukia yule mzee Mungu anisamehe tu [emoji119]
Hilo ndilo lililonifikirisha hadi kuanzisha uzi huu. Yaani mtu akiambiwa mpaka wa kiwanja chake ni kigingi, basi yeye anajenga mpaka kwenye kigingi hicho. Taabu kweli.
 
Watanzania tuna utamaduni wa kubanana sana. Ukiingia kwenye daladala, hakuna mtu atakayefanya jitihida za kutobanana, utakuta abiria anamwegemea abiria mwingine kila kupata ridhaa mradi tu "sote tubababe."

Bro ukitaka kujua watu wanabanana vipi kwenye public, nenda China au India...
 
Watanzania tuna utamaduni wa kubanana sana. Ukiingia kwenye daladala, hakuna mtu atakayefanya jitihida za kutobanana, utakuta abiria anamwegemea abiria mwingine kila kupata ridhaa mradi tu "sote tubababe."

Konda wa daladala anaweza kujaza abiria kuliko uwezo wa gari na kuwaacha wabanane na wala abiria hao hawawezi kulalamika.

Kwenye ujenzi wa makazi, utaona watu wanajenga mpaka kwenye mpaka wa kiwanja bila kuweka ile futi sita clearance kiasi kuwa mtu hawezi kupita katikakati ya viwanja viwili. Sababu yake ni nini?
1. Wanataka kutiana vidole
2. Kusoma sms na wenzao
3. Kutafuta umbea
4. Kunukishana harufu ya mdomo na Makwapa
 
Wewe sio Mbinafsi unapenda nature na utulivu, mimi pia next time tualikane mbugani na waterfalls,
Milimani hapana, nina phobia ya height (acrophobia) 🥲
Unaniogopa kama ukoma, nafurahi mwandiko wangu unakutisha, endelea kuniogopa😂😂😂
 
Deoforant ni 99% hawaijui
 
Back
Top Bottom