Kwanini Watanzania tunajenga utamaduni wa kubanana?

Bro ukitaka kujua watu wanabanana vipi kwenye public, nenda China au India...
China na India hawawezi kukwepa kubanana kutokana na idadi yao kulingana na ukubwa wa ardhi yao. Tanzania hatutakiwi tubanane.
 
Ni saikolojia ya umasikini. Ni kukosa maono ya kuweza kuona zaidi ya kilicho mbele ya macho yetu.

Tuna ardhi kubwa sana lakini tumejenga kwenye miji michache kwa kubanana.

Tuna uwezo wa kuzalisha cha kumtosha kila mtu, lakini wengi wanakufa kwa umasikini unaotokana na ujinga tu.

Katika kitabu cha "Why Nations Fail: The Origins of Power, Prosperity, and Poverty" waandizhi wamejadili mengi sana, lakini, kimoja cha msingi kabisa ni kwamba, nchi zilizoendelea zimejengwa katika misingi ya kumjumuisha kila mmoja, inclusivity.

Sisi tuna unhealthy competition. Tunafungiana fursa kwa njia za mkato ili wachache waweze kubaki juu.

Tunajikuta tunaua ubunifu.

Hapo hatuwezi kuendelea.
 
Hata kwako, mtu una nunua kitanda cha futi sita kwa sita ulalie hauridhiki unaenda kuoa mradi hiko kitanda mlale watu wawili mradi Mbabane tuuu, umezidi watanzania
 
Labda ni wapi ambapo public transport watu hawabanani?

Kuhusu makazi, ukishaamua kujenga kwenye unplanned places kubali usumbufu, kama hutaki nenda sehemu zilizopangilia.

Kuna sehemu inaitwa Tegeta Skansika, ile sehemu walokuwa wanachimba kokoto, kule likitokea na kutokea zimamoto lisiende maana nyumba zimeshikana na barabara hakuna. Kila mtu anajenga anavyojua na tamisemi ipo
 
Ujinga na kukosa ustaarabu
 
Hii imeathiri hata wafugaji, utakuta mtu ana kuku 500 ila banda aliloweka kuku Hao halina uwezo huo, zizi la mbuzi 100 mtu anaswaga humo mbuzi 500, wakati wa ukaguzi wa mifugo au chanjo anapita kwa shida yeye mwenyewe ili mradi tu afurahie kubanana banana mpaka na mbuzi.
 
Ujamaa umetutia ujinga flani ambao itachukua muda mrefu kuondoka.
 
We are black people, we are black people, we are black people!
They are not like us we are not like them.
Our physical appearance are quite different from them, why do you want to look, think and behave like them? We are different people.
Do you want a Monkey to look like Gorila, it will never happen until the end of the time.
Ipo siku utasema kwa nini tusioe kama wao.
Bob Marley aliwahi imba "we will share the shelter" kama unadhani aliimba ujinga shauri yako.
 
Public transportation haina maana ya abiria kubanana. In fact basi au tren linaweza kuwa limejaa lakini abiria hawagusani.

Hata maeneo yote yaliyopimwa ni yale ya low density tu ambayo hakuna mbanano. Ukienda Tabata, Segerea, Sinza, Goba kote nyumba zimebanana ingawa ni maeneo yaliyopimwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…