Kwanini Watanzania tunasema Jumapili ni mwisho wa wiki?

Kwanini Watanzania tunasema Jumapili ni mwisho wa wiki?

Lamzettttt

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2020
Posts
1,270
Reaction score
3,623
Habari za muda huu watu wote.

Nilikua naomba kufahamishwa ikiwa kimahesabu.. Mosi ni moja(2) kwa maana hiyo Jumamosi siku ya kwanza ya wiki, hivyo ni mwanzo wa wiki yenye siku saba.

Sasa inakuaje hapa Tanzania mwisho wa wiki yetu inakua ni kwenye pili (jumapili)?

Msaada Tafadhari!
 
Kwa sababu ni siku ya mwisho kabisa katika zile siku mbili za mapumziko yaani wikendi. Baada ya Jumapili tunaingia siku ya kwanza ya kazi (Jumatatu) na kuendelea na kazi hadi siku ya mwisho kufanya kazi rasmi (Ijumaa).

Matokeo yake Jumatatu inachukuliwa kuwa siku ya kwanza ya juma na Jumapili kuwa ya mwisho kimazoea.

Ila kikawaida Jumapili ndio siku ya kwanza ya wiki
 
Upo sahihi, chukua dictionary na utafute neno Sunday! Inasomeka kuwa Sunday is the first day of a week! Hujakosea hata kidogo!
 
Kiswahili ndio hivyo Mosi ndio ya kwanza kwahio mwisho ni Ijumaa kama vile ilivyo mwanzo wa saa ni asubuhi na sio saa sita usiku.

Anyway hizo zote ni man made na mapatano ya jamii husika tungetaka hata tungefanya wiki iwe na siku mbili tu na hakuna ambacho kingeharibika jua lingutuama kama kawaida
 
... inategemea unatazima from which angle. Inaweza kuwa last or first of a week depending on your perception.
 
Habari za muda huu watu wote.

Nilikua naomba kufahamishwa ikiwa kimahesabu.. Mosi ni moja(2) kwa maana hiyo jumamosi siku ya kwanza ya wiki ... Hivyo ni mwanzo wa wiki yenye siku saba.

Sasa inakuaje hapa Tanzania mwisho wa wiki yetu inakua ni kwenye pili (jumapili) ?

Msaada Tafadhari!
wiki yetu cc inaanza j3, hiyo habari ya jumamosi ni mapokeo tu ya kalenda zilizotengenezwa na wenzetu wa miaka ileeeeee!!!!!! ugiriki huko
 
Kuna weekend(Jmosi, Jpili) na weekdays (J3, J4, J5, Alh, Ijum)...
 
Kwahiyo ... Namba zetu zinaanza na tatu??
no zinaanza na moja kama kawaida, calendar ni jambo jingine tofauti kbs, jiulize tu kwanini mwezi febry una siku 28!!!, nani alisema iwe hivyo!!!!, pekua sana utagundua kwamba ni maamuzi ya watu fulani kulingana maisha yao wakati ule.
 
Habari za muda huu wewe mdau wa jamii forum? Shwari??

Kama juma lina siku saba. Na Siku ya saba ndio siku ya sabato. Maana yake jumamosi ni siku ya mapumziko . Na kama ni hivyo sasa jumapili ni siku ya kwanza ya wiki.

[emoji28]
 
Back
Top Bottom