Kwanini Watanzania wakikuona unavyo vingi wanataka mgawane?

Kwanini Watanzania wakikuona unavyo vingi wanataka mgawane?

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Hii tabia inaboa sana kwanza kwa Watanzania.

Yani ukiwa na simu zaidi ya tatu kila unapokwenda lazima ukutane na yeyote kwanini usinipe moja, wakati japo yeye anayo.

Ukiwa na gari zaidi ya mbili basi kama umetengeneza tatizo kwa wanaokuzunguka utasikia”una magari mengi bora ungetupa moja” sasa uliweka pesa yako.

Na vingine vingi jama Watanzania kila mtu na chake kukupa ni mimi kuamua.
 
Hapo kwenye magari ndipo niliteseka napo. Baba anaomba gari moja ampe mama. Kaka naye anaomba gari moja ampe mke wake (shemeji); Dogo naye anaomba gari moja 'atumie tumie'. Yani hapo mtu una magari mawili tu na moja la kazini lakini kero zilikuwa kama zote!
 
Duh huyo Nani huyo anaomba mpaka gari?

Me mwisho wangu ni bia

Haiwezekani me na arosto nataka malomoni halafu wewe uko mezani na chupa ya tano unakula vibe mwenyewe. Hapana kwa kweli niache nata mshikaji.
 
Kwani bandidos (Majambazi) wametoa kauli gani mpaka sasa?
 
Hao ndo wanaishiaga kufirimbwa ulembe
 
Hii ni kawaida inategemea unakaa mtaani au eneo gani.Ukiishi Masaki na Oyster bay huwezi kukuta mambo kama haya.Kuna mama mmoja Mwanza Capripoint alikwenda jirani kwa rafiki yake kumuomba chumvi ya mboga bahati mbaya aliishiwa.Baba mwenye nyumba alikuwepo kusikia hivyo akamuambia mfanya kazi wake ingia store uchukue ule mfuko wa kg25 umpe huyu mama yule mama alipokea vizuri lakini aliona kama amekejeliwa kuwa sehemu ile sio ya kuombana vitu.

Ukiishi uswahilini tegemea mengi ukiwa na gari sio la kwako unaweza amshwa saa nane usiku umpeleke mjamzito hospitali au upeleke msiba mahali flani. Ajabu sasa unaweza ukawa hujakataa lakini ukawa huna mafuta kwenye gari au gari lako limekwisha bima unaogopa fine barabarani au wewe mwenye gari huna leseni unatumiaga dereva wako siku zote sasa ukiwapa hizo sababu taryari wanaona umewakatalia.

Kuishi uswahili shida hata usipompa mtu lift anaona unaringa kumbe ndani ya gari una watu wengine lakini bahati mbaya hawaoni vile ni tinted. Dunia ndivyo ilivyo CHIZCOM huwezi kumridhisha kila mtu kikubwa utende wema unaweza kuutenda lakini huo wema usizidi uwezo maana hata ukitenda wema watakusema tu kuwa unajifanya unazo.
 
Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake ridhika na maisha ukiona nakula bata baada ya kupitia msoto mzito na gharama kubwa mafanikio yangu ni ya my wife na my kids, mtoa mada umeongea kitu kizuri sana.
 
Hata CCM wakiona WAPINZANI wanataka wagawane yaan waje CCM na wanawapa vyeo sijui kwann!!!
 
Back
Top Bottom