Kwanini Watanzania wako obsessed na Kenya?

Hivi ni mtanzania gani kaenda kenya kutafuta ardhi au lini Tanzania imetangaza vivutio vya kenya viko Tanzania nyie ndio mnahangaika na Tanzania ile ya kuzuia ndege ni mwanzo wa kuwaonyesha sisi ni nani hata mikataba mnayoforce itumike East Africa mingi tunaikataa sababunataka kujiingiza nchini mwetu kijanja
 
Kaangalie mikutano ya Lowasa alipokua ukawa.
Tz huijui

Tatizo kwa Lissu hamuwezi kutumia goli la mikono, atawasumbua sana, sio mwoga mwoga, amelishwa risasi 38 na bado anapeta, huo ujasiri dadadeki zake siuwezi, hapo hata ngosha anaingiwa na kauwoga fulani.
 
hajapatikana wa kumtoa magufuli madarakani.hivyo jiandaeni kwa miaka 5 mingine ya kunyooshwa ukanda huu.

sisi hatuchagui kelele kama hapo kenya,tunaangalia kichwani kuna nini.

Sasa hapo kwa kichwani ndio mtakua mumeingia 18 zake, mumeogopa hata mdahalo naye, kila siku mnahangaika kujibu hoja zake hadi mumehema, kwanza naona kawatoa kamasi kwenye suala la machinga, hapo ndio mnaangukia pua mchana kweupe.

Dah! ila hata Wakenya tujiandae mkao wa ushindani mkali Lisu akichukua uongozi, kwa mara ya kwanza Tz itaongozwa na mtu kichwa, msomi, mjasiri na anayethubutu asiye mwoga mwoga, anaweza akaipaisha Tanzania hadi watufikie ndani ya muda mfupi, bora kidumu chama cha kijani.

Pona yetu Tanzania imejaa hawa hapa 66%

 
Tatizo kwa Lissu hamuwezi kutumia goli la mikono, atawasumbua sana, sio mwoga mwoga, amelishwa risasi 38 na bado anapeta, huo ujasiri dadadeki zake siuwezi, hapo hata ngosha anaingiwa na kauwoga fulani.
Wote ni watanzania wanayo haki ya kusikilizwa na kuchaguliwa na watanzania, usijaribu kutugawa, sisi tunataka maendeleo kama anayotufanyia Magufuli, usijenge picha kwamba hapa ndani wote ni CCM, sisi ni watanzania japo kila mtu anayo mapenzi kwa chama au mgombea wake.

Hawa hawa walikua wakimnanga Kikwete kutokana na ulegevu wake na tabia yake ya kupenda kusafiri nje ya nchi. Hawahawa sasa hivi wanamkubali Magufuli kutokana na uimara wake wa kujenga uchumi. Haijalishi chama alichotoka, kama Lisu atapita na kutuletea maendeleo, tutamuunga mkono, ila akileta za kuleta, lazima tumshukie.
 
18 threads out of 24 on the first page of Kenyan news and politics(50% by geza ulole) are posts by Tanzanians and they are all about why Tanzania is better than kenya or why kenya is doomed, hamna hata ya kupromote Tz in good spirit.
 

hivi rais wa nchi ana mda wa kipuuzi eti anakaa kubishana na mtu!!!!labda kenya ndio mna huu ujinga.miaka 5 hii mmeona jinsi tz inatakiwa kuwa miaka yote,subirini aapishwe kwa mara ya pili tuendelee kuwavuruga vuruga kama mchicha.

huyo lissu wenu sio msubiri tu ashinde huku hawezi kushinda,cha kufanya mchukueni mumpe uraia agombee mumpe nchi huko kwenu atawafaa sana.
 

Anaweza akawapa tabu sana kwenye mdahalo atawaumbua maana mumezoea kueleza bila kuhojiwa kauli zenu, yaani kwenye mdahalo unakalishwa kwenye kiti moto, unahojiwa ulivyoboronga kwenye korosho na kuacha wakulima wakiteseka, mindege umenunua isiyokua na tija, uchumi kwenye awamu ya tano ndio umekua kuliko awamu zote, madeni mumechukua kutoka kwa mabeberu kuliko awmu zote yaani kuna mengi mnaweza mkalishwa za uso, duh hata msithubutu, kaeni mbali na habari za mdahalo, nyie ongeeni huko kisukuma na kutegemea kete ya ukabila.
 

huo ni mtazamo wako,kama ana uwezo wa kuongea asingesumbuliwa na mtangazaji kwenye interview na shirika la uingereza.

kuna tofauti kubwa sana kati ya kuongea unayohisi ni sahihi ukiwa peke yako,yule hata pole pole hamuwezi.
 
huo ni mtazamo wako,kama ana uwezo wa kuongea asingesumbuliwa na mtangazaji kwenye interview na shirika la uingereza.

kuna tofauti kubwa sana kati ya kuongea unayohisi ni sahihi ukiwa peke yako,yule hata pole pole hamuwezi.

Kwanza mumepoteana hadi huyo Pole Pole anaitisha press conference kila siku kujaribu kujibu hoja za Lissu....hehehehe!
 
Kwanza mumepoteana hadi huyo Pole Pole anaitisha press conference kila siku kujaribu kujibu hoja za lissu....hehehehe

Ndio mikakati ya ccm hiyo kucheza na akili za wapinzani mazuzu.

Subiri ushindi wa 85% ndio utajua hujui.
 
Kenya sasa hivi wanadai Simba ni timu yao yaani hawaonagi aibu kujifanya vitu vys wenzao ni vya kwao.
 
Nakubaliana na wewe .unajua mtu ambae hajiamini ana tabia ya kuhangaika sana.sasa Sisi watanzania tunataka kutambulika na namna pekee iliyobaki katika ukanda huu wa Africa mashariki ni kuendelea kubishana na wakenya ambao atleast tunashea mambo mengi ukanda huu .na ukizingatia Kenya mumeendelea kutuzidi.
 
Ndio mikakati ya ccm hiyo kucheza na akili za wapinzani mazuzu.

Subiri ushindi wa 85% ndio utajua hujui.

Labda kwa mabomu ambayo naona mumeanza kumpiga. Jamaa atawazingua sana, kwanza amekaidi agizo la kwenda mbele ya tume la maadili, sijui mtatumia kete gani nyingine.
 
Labda kwa mabomu ambayo naona mumeanza kumpiga. Jamaa atawazingua sana, kwanza amekaidi agizo la kwenda mbele ya tume la maadili, sijui mtatumia kete gani nyingine.
Huku ni kukosa busara kwa hali ya juu Sana, hivi inakuaje mtu kutoka nchi jirani unaamua kuchukua upande na kushabikia upande mmoja wa siasa katika nchi nyengine?, lengo lako hasa ni lipi?.

Kwahiyo kama CCM au Magufuli ataona kwamba wakenya wanashabikia upanzani na akifanikiwa kurudi madarakani unataka awachukuliaje wakenya?. Tumia busara kidogo, huu ushabiki hapo ni kati ya Kenya na Tanzania, tatizo lenu kwa muda mrefu mumekua mkichukulia kwamba mtu yeyote mwenye kusifia utendaji wa serikali ya Tanzania huyo ni CCM.

Hii inaonyesha wazi jinsi Jubilee wanavyokichukia CCM na Magufuli. Tumia busara kutokujiingiza katika siasa za kishabiki za nchi jirani, hukatazwi kutoa ushauri, lakini sio kushabikia upande mmoja.
 
Busara gani wakati nyie kwanza wewe ukiwa mmoja huwa unaiponda Kenya sana.Nashangaa unalia nini sasa.Kiongozi wenu ameonyesha mara kadhaa kuchukia Kenya na Wakenya.Yeye na wafuasi wake hapa(miccm) wameadhirisha hilo.Heri Kikwete lakini for now as a Kenyan am with Lissu 💯.Yeye hana chuki dhidi ya Kenya wala wakenya
 
Unapaswa utulie na upunguze mihemko yako, hapa ni kati ya Kenya na Tanzania, sio kati ya Jubilee na CCM. Mkenya kuiponda Tanzania na mtanzania kuiponda Kenya hiyo ni sawa kabisa.

Sisi huku tunaiponda au wale wanaoisifia Kenya haina maana kwamba ni kutoka upande mmoja wa siasa. Mimi ninaamini wapo CCM wanaoisifia Kenya, na wapo Jubilee wanaoisifia Tanzania.

Hapa ni kati ya Kenya na Tanzania, haina mana kwamba kila mtanzania anayeipenda na kuisifia Tanzania na kuiponda Kenya, basi lazima ni CCM.

Kumbuka watu hawahawa ambao wanamsifia Magufuli na Tanzania, ndio ambao tulikua tunamshambulia Kikwete pamoja na kwamba alikua ni rais toka CCM. Kwa kumshabikia Lisu haina maana hata akiingia madarakani watanzania wataacha kuishambulia Kenya, uzalendo wa nchi yetu utabaki pale pale.
 

hakuna mtu hawa panya wanamchukia kama magu.

amewafanya vibaya sana,wanajihisi wako uchi.

unawezasema ni kweli wana maono positivu kumtaja lissu kumbe sio,wanatamani aingie mwingine mpuuzi waendelee upuuzi wao.
 
If hate is obsession ni sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…