Kwanini watanzania wana tabia ya kukomenti kwa maneno ya ovyo kwenye mitandao ya kijamii?

Malezi ya mtoto wa kitanzania yamejaa maneno ya kudunisha, matusi na kejeli toka kwa wazazi, ndugu, walimu na majirani.

Mtoto akiuliza swali, anaambiwa "n'tolee ujinga wako hapa" au "bichwa kubwaaa, akili huna".

Kimsingi, watanzania wengi wako traumatized na childhood experiences.

Je utategemea kupata majibu ya upendo toka kwa watu waliokuzwa kwa kejeli, chuki, masimango n.k?
WELL SAID.

Wengine mpaka tumeambukizwa MAKOMWE kisa kufokewa

Depal

binti kiziwi
 
Ni ugeni wa mitandao, yaani unamwandikia mtu mwingine asome hoja huku mtu huyo HAMFAHAMIANI ! inahitaji kuwa na malezi ya kizazi cha kuandikiana BARUA.

Kizazi cha kuandikiana barua , kununua bahasha , karatasi au airform na stamp kusafiri hatua kadhaa kwenda Posta kisha kusubiria majibu baada ya siku kadhaa .

Ilitosha kujifundisha ADABU kwa hii mitandao.
 
SAHIHI.

Kizazi cha TIK TOK kina matusi haswaaa

cc mshamba_hachekwi
 
Malezi ya mtoto wa kitanzania yamejaa maneno ya kudunisha, matusi na kejeli toka kwa wazazi, ndugu, walimu na majirani.

Mtoto akiuliza swali, anaambiwa "n'tolee ujinga wako hapa" au "bichwa kubwaaa, akili huna".

Kimsingi, watanzania wengi wako traumatized na childhood experiences.

Je utategemea kupata majibu ya upendo toka kwa watu waliokuzwa kwa kejeli, chuki, masimango n.k?
😭😭😭😭😭😭
 
Watanzania wengi wana kaushamba ka kutoa maoni kwenye mitandao ya kijamii.

Sehemu Pekee wanacomment kwa adabu ni post za Vifo vya ajali hususan ajali za barabaran

Lakini post nyingine zote wanatoa maneno ya chuki na roho mbaya

Wenzetu ulaya wanacomment kwa adabu hâta kwa wale wacheza picha za ngono etc.
CHAI
 
Msongo wa Mawazo ndo chanzo kikuu
 
Mtoto akiuliza swali, anaambiwa "n'tolee ujinga wako hapa" au "bichwa kubwaaa, akili huna".

Kimsingi, watanzania wengi wako traumatized na childhood experiences.

Je utategemea kupata majibu ya upendo toka kwa watu waliokuzwa kwa kejeli, chuki, masimango n.k?

I cement this! Na huko tuendako ndipo pabaya zaidi. We are all surrounded by traumatized people, who have nothing good to say about others.

Mbaya zaidi wengi wetu tuko very opinionated, hatuna ufahamu wa jambo gani la kulitolea opinion na jambo la kumind our business. Yaani mtu anaweza kukomaa kutoa mawazo yake kumkosoa msanii lakini mwanasiasa akifanya blunder hapa wanapita kama hawaoni.

Tujifunze jamani, kama hujaombwa maoni, kama hujaalikwa na kama kitu hakihusu KODI yako, sio lazima kuwa opinionated, tujitahidi kujua wapi pakukomaa wapi pakufuata mambo yetu.

Hatufahamu tofauti ya kutoa maoni na kufanya bullying.

Kazi kubwa sana inapaswa ifanyike juu ya jamii ya waTz.
 
Hatujajifunza kutoka Kwa ushauri alioutoa akitoka Villa tulikomharibia ulaji
 
Samata tulitusi Aston Villa ikabidi aondoke....Kisha tunarudi vijiweni meno yote nje....akili yetu(???) Tunajua wenyeww je Hizi ni akili kweli [emoji45]
 
I cement this! Na huko tuendako ndipo pabaya zaidi. We are all surrounded by traumatized people, who have nothing good to say about others.

Mbaya zaidi wengi wetu tuko very opinionated, hatuna ufahamu wa jambo gani la kulitolea opinion na jambo la kumind our business. Yaani mtu anaweza kukomaa kutoa mawazo yake kumkosoa msanii lakini mwanasiasa akifanya blunder hapa wanapita kama hawaoni.

Tujifunze jamani, kama hujaombwa maoni, kama hujaalikwa na kama kitu hakihusu KODI yako, sio lazima kuwa opinionated, tujitahidi kujua wapi pakukomaa wapi pakufuata mambo yetu.

Hatufahamu tofauti ya kutoa maoni na kufanya bullying.

Kazi kubwa sana inapaswa ifanyike juu ya jamii ya waTz.
Ni ngumu kulitibu KUNDI LA NYUMBU MILIONI 60 👀

Unajua NYUMBU ni kama MAZOMBI, ukimfyatua mmoja wanakuja wengine mia saba, hawaishagi sijui kwanini!

Zile movie nazo!!! Ndo maana mama mkwe hapendi kuziangalia. 🙈🙈
 
Wengi wanaenda ku trend kwa ujinga. Wengine ni kutoa stress. Wengine ndivyo walivyo. Wengine ni kutaka kuonesha umwamba wa jambo fulani tu. Ila mara nyingi ni ujinga hata humu JF tunao wajinga wengi tu au wanaojifanya wajinga
 
Back
Top Bottom