Kwanini Watanzania wengi hatupo huru kuonyesha hisia zetu hadharani?

Kwanini Watanzania wengi hatupo huru kuonyesha hisia zetu hadharani?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Ni kama vile hisia zetu zimefungwa gerezani kwasababu ya hadhara, na pake mtu anapokuwa huru kuonyesha hisia zake maswali yanaanza kwamba ni kichaa ama kalewa.

- Muziki unapigwa unaoupenda lakini unajizuia kuufatisha au kucheza huku miguu imedinda inataka kuruka ruka.

-Kitu kimekuchekesha mpaka basi lakini unajibana kucheka kisa kuna watu tena ambao hata hawakujui.

-Chakula chako unachokipenda kama pilau kuku unajivunga kuweka kiasi kinachokutosha ama kurudia raundi kwa kuogopa watu.

n.k
 
Mi nikiona dada ana mzigo amepita, sijizuii kuangalia na kutikisa kichwa.
 
Mi nikiona dada ana mzigo amepita, sijizuii kuangalia na kutikisa kichwa.
kama vipi unamwambia kabisa kabarikiwa, unakua umeipendezesha sana siku yake, nani hapendi kusifiwa aisee ?
 
Kwasababu tumelelewa kuiogopa jamii
hii ni shida, kuna siku gari ya matangazo imepita inapigwa ngoma ya muziki ya darasa mzuka ukanipanda nikaanza kucheza, aliekuja kuniunga ni jamaa flani tu kalewa, wengine naona wanatamani kucheza ila wana hofu
 
Nadhani hapo umejizungumzia wewe na wala sio watu woote

Kuna watu wanaweza kufanya hayo yoote uliyo andika bila uoga wowote.
 
Back
Top Bottom