Ni kama vile hisia zetu zimefungwa gerezani kwasababu ya hadhara, na pake mtu anapokuwa huru kuonyesha hisia zake maswali yanaanza kwamba ni kichaa ama kalewa.
- Muziki unapigwa unaoupenda lakini unajizuia kuufatisha au kucheza huku miguu imedinda inataka kuruka ruka.
-Kitu kimekuchekesha mpaka basi lakini unajibana kucheka kisa kuna watu tena ambao hata hawakujui.
-Chakula chako unachokipenda kama pilau kuku unajivunga kuweka kiasi kinachokutosha ama kurudia raundi kwa kuogopa watu.
hii ni shida, kuna siku gari ya matangazo imepita inapigwa ngoma ya muziki ya darasa mzuka ukanipanda nikaanza kucheza, aliekuja kuniunga ni jamaa flani tu kalewa, wengine naona wanatamani kucheza ila wana hofu