Kwanini watanzania wengi wanafurahia kwa kupigwa Hassan Mwakinyo

Kwanini watanzania wengi wanafurahia kwa kupigwa Hassan Mwakinyo

Kheri zitawale

Zilianza taarifa kuwa hakuwa akipewa sapoti za kutosha na baadhi ya watu na media, kama mtanzania wanadai alitakiwa apewe sapoti na media zote nchini binafsi najua hizi media ni zinafanya biashara na zikiona hazipati chochote haziingii kwenye biashara ya mtu mwingine

Nasikitika tu kwa watu/raia wa tanzania na watu maarufu kumsusia jamaa kwa kutompa sapoti

Labda anaponzwa na bwebwe zake za kujiamini kupita kiasi na maneno yanayomchacharika mdomoni ya shombo la samaki… natania

Mabondia wenzake wengi huyu jamaa hawamtaki na sio kwa sababu ya ubora wake ni mambo yao wenyewe binafs

Ikiwalinganisha na mabondia wa tanzania wengi viwango vyao havipishani sana ila ni ana uongozi mzuri jamaa hicho anabidi ajivunie sana wanaomuongoza wanajielewa sana na wanachangia kipaji chake kuwa cha kipekee

Labda mafanikio yake au maneno yake ya kuringa na kujihisi ni wa kipekee, ndicho kinachomfanya wengi wa mabondia wenzake wamchukie

Taifa tusimameni na wanamichezo wetu

Soma Pia BOXING: Michael Soro amchapa kwa TKO Hassan Mwakinyo. Pambano limechezwa Parc Des Expositions, Abidjan, Ivory Coast. Juni 11, 2026
Hata kushangiliaa tu kuanguka kwa binadamu mwenzio ambae hata kukujua hakujui,anapambana kutafuta riziki yake ya halali ni Uchawii tu kama wachawi wengine.
 
Huyo ni kama Samara alivyoenda
Mjuaji au anapigania maslahi

Ova
Kila mtu anapigania maslahi.
Ila yeye hajielewi.
Sasa kupigwa na soro na kupigwa na twaha kiduku Kuna tofauti gani?
Unadhani huko amepewa shilingi ngapi?
 
Watz Bana sasa hapo kinachowafurahisha watu ni nini?, ule si mchezo Tu kuna kupiga na kupigwa...Mbona tuna roho za kichawi namna hiyo. Mtu hata hakujui.
 
Back
Top Bottom