Sijui hata niwekeje ila
Maji ni moja state of matter ambayo inamfanya mtoto kua curious na kua na interest nayo sana kutokana na sifa yake,
Naomba nitumie kimombo kidogo.
Stimulation : Mtoto akiweka mkono kwenye maji, ile sense of touch inamvutia, ile Sauti ya kuchuruzika akiisika anaifurahia, akichezesha vile yanavyozunguka anafurahia.
Freedom of Control: Maji ni kitu pekee ambacho mtoto anaweza akaki Control kirahisi, anaweza akayafanya kivyovyote anavyotaka,
Physical activity: Mtoto Kucheza na maji kunampa option nyingi sana za Physical exercise mfano kuyahamisha, kuyarusha kwa kutumia chombo au mikono, kujimwagilia, kutengenezea kitu, kuyaweka kwenye chomcho chochote, kujimwagi(kuyaoga) n.k, uhuru wa kuyafanya hivyo na kumpa michezo mingi kwa pamoja kunamfanya ajihisi furaha na kuona ndio mchezo wake mkubwa.
Curiosity/Exploration/Discovery: Maji yanamfanta mtoto ajiulize maswali mengi sana,
Kuna mda anaweka kitu kinaelea, kwa nini?
Akiyamwaga chini yanachuruzika, kwa nini?
Akiyachezea na mkono yanaruka,kwa nin?
Haya sasa, kwa nini kwenye Kuogeshwa hii habari inageuka kabisa.
Hana ule uhuru tenaa..
Anajihisi sio salama anapokua Uchi,
Hawapendi ile hali ya mabadiliko ya ghafla ya joto la mwili, mfano unapomvuanguo ule ubaridi au maji yanapomwagikia.
Kumkatizia uhuru/mcheozo aliokua anafanya
Kumbukumbu za nyuma, mfano mtoto alishaingiwa na maji/povu machoni n.k, hivyo hujenga hofu.
Haoni umuhimu wake, unapomuogesha mtoto suala la usafi na uchafu ni kwako, yeye anachoona unamnyanyasa na kumkatishia mambo yake mengine sababu ya wivu wako.