Kwanini watu hugombania kuzika maiti?

Kwanini watu hugombania kuzika maiti?

Habari za mchana wanajamii forums.?
Nisiwapotezee muda, niende moja kwa moja kwenye mada.

Kuna swali huwa ninajiuliza sana lakini bado sijawahi kupata jibu halisi, ninaomba mwenye uelewa wa hili swali anipe majibu.

Ni mara nyingi huwa tunaona ama kusikia matukio ya aina hii, watu kugombea maiti. Unakuta wengine wanataka marehemu azikwe kimila wengine wanataka azikwe kidini au wengine wanataka akazikwe kwao wengine wanataka azikwe alipofariki yani unakuta ni vurugu mwanzo mwisho.

Faida yake huwa ni nini.?
Mshana Jr
Rakims
jerryempire
  1. Mila na desturi za maziko ya ukoo wao
  2. Mirathi ya marehemu
  3. Ushamba
  4. Ushirikina
  5. Kuoneshana nguvu ya hela
  6. Ongezea mengine
 
Fafanua hapo mkuu
Kizaa zaa chenyewe kipo pale ambapo umeoa binti ya watu na akafa wakati hujamtolea mahari, Aisee utaona Cha Moto Sana haya mambo yapo vijijini watu wanapigana mapanga kiss tu ugomvi wa maiti.
 
Sana sana ni kaburi liwe karibu na ndugu wa karibu. Wengine huwa sio ndugu wa karibu sana. Mfano mke akifa ndugu zake watataka azikwe kwo, hali kadhalika mume naye akifa ndugu zake nao watataka azikwe kwao.
 
Habari za mchana wanajamii forums.?
Nisiwapotezee muda, niende moja kwa moja kwenye mada.

Kuna swali huwa ninajiuliza sana lakini bado sijawahi kupata jibu halisi, ninaomba mwenye uelewa wa hili swali anipe majibu.

Ni mara nyingi huwa tunaona ama kusikia matukio ya aina hii, watu kugombea maiti. Unakuta wengine wanataka marehemu azikwe kimila wengine wanataka azikwe kidini au wengine wanataka akazikwe kwao wengine wanataka azikwe alipofariki yani unakuta ni vurugu mwanzo mwisho.

Faida yake huwa ni nini.?
Mshana Jr
Rakims
jerryempire
Kuna maslahi baada ya marehemu kuzikwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom