Kwanini watu wakiacha pesa zao benki kwa muda mrefu akiba yao ndiyo inakatwa badala ya wao kupata faida?

Kwa NMB Mobile Bank kulipia Bills za Maji,Umeme,TRA na kununua muda wa maongezi katika simu wanakata Pesa nijulishe mkuuu
 
Kwahiyo wewe unaoona huo utaratibu wa kukata hela kweye akiba ya mtu ambaye kaziacha tu ni sawa?

Siyo kila utaratibu uliowekwa na haya mabenki uko sawa,moja wapo ni huu uondolewe
Mtoa mada yuko sahihi sana.
Hata Mimi inaniboa sana kuweka hela benki.
Labda pesa kuanzia milioni 5 kwenda mbele ndio huwa nawaza kupeleka benki.
Vinginevyo ni hasara tupu.
Ukipiga mahesabu ni hasara tupu.
 
nenda kaweke equity bank, hawana makato
 
nenda kaweke equity bank, hawana makato

Nashukuru Mkuu, huko nna akaunti ya USD. Hawana makato ya kila mwezi, unakatwa unapofanya muamala tu.

Tatizo hawana ATM kwa hizo USD ambapo sio tatizo sana kwa upande wangu.
 
In a big picha ...

Kabla hujaweka fedha bank ni vema ukajiuliza, kwanini hizi hela nisikae nazo mwenyewe mfukoni ama nyumbani?

Zipo baadhi ya nyakati ni bora kubaki na hela zako mfukoni ama nyumbani kuliko kuzipeleka bank, kwa mfano:

- Kama una hela kidogo sana
- Kama gharama ya kuziweka bank ni kubwa kuliko ile ya kuzitunza mwenyewe

Sasa basi:

(1) Kama sababu kuu ya wewe kupeleka fedha bank ni ili bank ikusaidie kuzitunza coz ukikaa nazo unaogopa kuzipoteza ama kulia bata then hapo lazima uwalipe kidogo kwa kukulindia, kumbuka, wataziwekea bima na ulinzi wa kimazingira pia

(2) Kama unapeleka ili upate faida zaidi then, waambie na watakuelekeza kwa kiasi ulicho nacho hata kama ni kidogo ni kwa asilimia ngapi wanaweza kukufidia kwa kukaa na fedha zako

- Mwisho, kwenye kila bidhaa ya kibenki huwa kuna terms na conditions .... ukiweza, pata muda kuzisoma kabla ya kujiunga

Usiende tu bank kama unaingia super market kwamba chochote kitakachokuvutia utanunua
 
🚶‍♂️ 🚶‍♂️
 
Iyo pesa ya kutolea 900 na list au bila list
Nijulishe
 
Mobile money ni nzuri ila makato yake sasa kwenye kutoa na kutuma
 
Account gani iyo mkuu, ndo saving account au vipi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…