Kwanini watu wanahoji uteuzi wa wagombea wa CCM?

Kwanini watu wanahoji uteuzi wa wagombea wa CCM?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Mwl. Nyerere aliwahi kusema, "kama CCM ikimtangaza mgombea wake huyo ndiye atakaekuwa Rais". Hivyo alitaka wagombea wa CCM wajulikane mapema ili watu wapate muda wa kuwajua na kuwajadili kwa muda mrefu kabla ya kuteuliwa na kabla ya siku ya uchaguzi. CCM wamefanya hivyo alhamdulilah kwa wagombea wao wa 2025.

Shida ni moja tu, kwakuwa mgombea wao alikuwa Rais aliyepatikana kwa mujibu wa katiba baada ya Rais mwenyewe aliyepitishwa kwenye kura za maoni kufariki dunia, wagombea wao hawa wa 2025 walipaswa pia kupitishwa kwenye mchakato wa mchujo wa kura za maoni ili wananchi waseme sawa au hapana miongoni mwa majina mengine. Maana aliyekuwa amepitishwa kwenye kura za maoni alikuwa DR. Magufuli (RIP).

Viongozi hawa wanafaa maana tunawafahamu kazi na utendaji wao, lakini hawakufuta utaratibu wa kura za maoni, hawakupita kwa wananchi Wala kushindanishwa na watia nia wengine kama inavyotakiwa kwa Kila mtu anaetaka au kutamani kuwa Rais wa nchi hii.
 
Baada ya Katiba kutusaidia kutuvusha katika kipindi kigumu cha kufiwa, sasa tulitakuwa kurudi kwenye taratibu zetu tulizozizoea za kupata mgombea Tena.
 
Back
Top Bottom