Kwanini watu wanamshambulia Jaji Warioba badala ya kupinga hoja zilizowasilishwa kwa hoja mbadala?

Kwanini watu wanamshambulia Jaji Warioba badala ya kupinga hoja zilizowasilishwa kwa hoja mbadala?

Kama umewasikiliza akina Wasira na Kingunge wakiwa TBC1 wamempinga Warioba kwa hoja. Sema tu hupendi warioba akosolewe. Huwezi kutatua matatizo ya ndoa kwa kuongeza idadi ya wanawake

Hebu nambie kuna kundi gani lingine linalo pinga hoja za warioba zaidi CCM?

kasome waraka makini kuhusu swala zito la Muungano kutoka kwa askofu Paul Ruzoka na kikundi chake cha CPT utabadili mwelekeo hata Mimi nilikuwa kama wewe lakini hotuba ya warioba na ule waraka ni habari ya serikali 3 .utaelewa tu.
 
CCM imeamua kuweka pamba masikioni, ikaamua kuvaa miwani ya mbao ili hoja za kuwa na serikali 3 zisipate nguvu. Huu ni upu..zi wa hali ya juu kabisa. ukisoma historia ya Muungano kama ilivyoandikwa ndani ya nyaraka mbalimbali za nchi hii kuna kila sababu ya kuwa Muungano wa serikali 3. Jaji Warioba ametukumbusha mbali. Ameturudisha enzi za Nyerere na Karume, Mzee Jumbe, G55, Jaji Nyarali, Jaji Kisanga, Tume ya Amina na sasa Jaji Warioba. Ukweli umeelezwa bila chembe ya chuki, unafiki wala woga. Hakika Warioba amejikita kwenye Dira ya Tume, Maslahi ya Taifa. Amejitenga na wanachama wenzake CCM kaamua kusema ukweli. Siku moja ataitwa Baba wa Taifa Jipya, Tanganyika! Tutamkumbuka sana!
 
Kama umewasikiliza akina Wasira na Kingunge wakiwa TBC1 wamempinga Warioba kwa hoja. Sema tu hupendi warioba akosolewe. Huwezi kutatua matatizo ya ndoa kwa kuongeza idadi ya wanawake

Issue ni kwamba je hoja zao zilikuwa sahihi?
 
Kama umewasikiliza akina Wasira na Kingunge wakiwa TBC1 wamempinga Warioba kwa hoja. Sema tu hupendi warioba akosolewe. Huwezi kutatua matatizo ya ndoa kwa kuongeza idadi ya wanawake

Nadhani hapo kwenye bold ndo hoja kuu ya ccm, zaidi ya blah blah hawawezi kuja na hoja makini.
 
Back
Top Bottom