CCM imeamua kuweka pamba masikioni, ikaamua kuvaa miwani ya mbao ili hoja za kuwa na serikali 3 zisipate nguvu. Huu ni upu..zi wa hali ya juu kabisa. ukisoma historia ya Muungano kama ilivyoandikwa ndani ya nyaraka mbalimbali za nchi hii kuna kila sababu ya kuwa Muungano wa serikali 3. Jaji Warioba ametukumbusha mbali. Ameturudisha enzi za Nyerere na Karume, Mzee Jumbe, G55, Jaji Nyarali, Jaji Kisanga, Tume ya Amina na sasa Jaji Warioba. Ukweli umeelezwa bila chembe ya chuki, unafiki wala woga. Hakika Warioba amejikita kwenye Dira ya Tume, Maslahi ya Taifa. Amejitenga na wanachama wenzake CCM kaamua kusema ukweli. Siku moja ataitwa Baba wa Taifa Jipya, Tanganyika! Tutamkumbuka sana!