Kwanini watu wananunua gari Japan?

Tony Yeyo

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2014
Posts
729
Reaction score
555
Watu wananunua Magari used Japan kwani hakuna nchi nyingine ambayo unaweza agiza gari kwa bei nafuu?

Sijaelewa kwanini Magari mengi used yanatoka Japan!
 
1. Japan kuna idadi kubwa ya magari Used but excellent Quality
2. Japanese government imerasimisha biashara ya exportation ya magari used.
3. Kuagiza gari used Japan ni rahisi sana., kila kitu unafanya online.
4. Magari used Japan ni very Cheap..
5. Upatikanaji wa Spares za magari ya kijapani ni mkubwa hapa Africa..
6. Mafundi wanaoweza kutengeneza magari ya kijapani ni wengi sana hapa Africa(na kwengineko)..
6. Matunzo ya gari za 'mjepu' ni gharama ndogo sana hivyo yanatufaa sisi waafrica.. kama hauamini nunua BMW, Benz.. etc uje ufungue uzi wa kulialia hapa..
7. Japan ina raia zaidi ya mil 150 wenye vipato vikubwa, hivyo kuna idadi kubwa sana ya magari used maana karibu kila mtu ana gari na kila baada ya muda mfupi atataka kubadili.
8. Kutokana na biashara hii kujikita mizizi (point 2 hapo juu), Usafirishaji wa magari kupitia meli kwenda maeneo mbalimbali duniani ni wa rahisi na uhakika..
....Kwenu Studio
 
Japani ndio nchi inayoongoza kwa kuzalisha magari duniani... kwahyo kule gari ni kama unaenda baharini kuvua samaki... gari za japan ni bei rahisi na vifaa vyake bei rahisi inawafaa maskini na matajiri... gari za ulaya mpaka uwe na mahela mengi sana
 
Kwann sio rahisi kununua gari used lililotumika Malawi, Kenya au nchi jirani na Tz
 
Point namba sita ni kwa wakata ufuta tu ndiyo watalialia binafsi sijawahi kumiliki Japanese vehicle na sijawahi kulialia...kupanga ni kuchagua. Japan ina MoU na nchi nyingi hasa za Africa...baadhi ya nchi za West Africa they don't import from Japan majority ya magari yao wanaagiza nchi za ulaya
 
Kwann sio rahisi kununua gari used lililotumika Malawi, Kenya au nchi jirani na Tz

Gari hilo tayali linakua limeshatumika huko japan na pia likiwa malawi,kenya ujue limetumika tena kwahio haina maana ununue double used ya Japan na africa.
 
Gari hilo tayali linakua limeshatumika huko japan na pia likiwa malawi,kenya ujue limetumika tena kwahio haina maana ununue double used ya Japan na africa.
Kwan kuna tatizo gani nikivuka nchi jirani nikamtafuta dalali akanitaftia gari nikalipenda nikavuka nalo, kwann haiwi hivyo?
 
Kwan kuna tatizo gani nikivuka nchi jirani nikamtafuta dalali akanitaftia gari nikalipenda nikavuka nalo, kwann haiwi hivyo?
Huko ulikotaja tuagize sio wazalishaji, japani anazalisha pia watu wa japan wanatunza magari sio kama hao uliowataja majirani zetu
 
Kipenda Roho Hula Nyama Mbichi

Kipenda Roho Haambiwi Wala Haoni

Hongera bob..
 
Actually Japan ina watu 123+ milioni hawajafika huko 150+population.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…