Kwanini watu wanaogopa kupima VVU?

chanawalleti

Member
Joined
Jul 16, 2016
Posts
49
Reaction score
45
Nilienda kupima vvu last month nilivyofika pale jinsi tuu nilivyokua najiamini hadi yule mhudumu alishangaa tulipiga stori kama ndugu badae nikapokea majibu nipo positive akanipa rufaa kwenda kitengo cha dawa arvs pia nilipofika pale yule mhudumu tulipiga stori sana alikua anashangaa ni jinsi gan najiamini nikapima uzito urefu, cd4 nk.

Baada ya siku nikaenda kuangalia cd4 nikaanza dawa nikapata somo la dawa nilichojifunza na kila napoenda pale asilimia ya wagojwa wengi wanaokuja kuchukua dawa pale wanaogopa pia wanasubiri mpaka kinga ishuke sana niliona kweli watu.

Wamekonda balaa maana tayari washapata magonjwa nyemelezi, pia wengi wana acha dawa kiukweli nimejifunza kitu kutokana na hizi dawa maana ukizimeza huwa unakua kama unachanganyikiwa.

Unaona vitu vya ajabu ajabu sana pia hizi dawa vidonge ni vikubwa mno vinatisha, pia hizi dawa ukinywa kama hujala utajuta pia nilichojifunza watu wengi wengi huogopa sana kwenda kuchukua dawa wakiona kua wataonekana na watu wanaowafahamu ila ushauri ni kujitokeza na kupima afya yako na kuanza dawa mfano mimi nilivyo now mpaka mtu ujue natumia ni vigumu sana.
 
Ujasir kujiamin na kukubal matokeo...walioweng hawana ujasir wa kukubal matokeo yako....
 
Hadithi yako inatufundisha kitu gani!?
 
Hawaogopi kupima ila wanaogopa majibu mabaya, kama mpimaji angehakikishiwa majibu mazuri baada ya kupima basi kila mmoja angepima.
 
Kuleta uu uzi tu hapa inaonyesha umelikubali suala hilo na pia hii ni sehemu ya kupata relief pia

Watu wanaogopa sababu ya propaganda na nadhalia nyingi za uongo na kukatisha tamaa huku wanasahau kila mtu atakufa na haijalishi kwa staili gani
Siku hizi ajali zinaua sana kuliko wakati mwingine wowote
 
Kama Wewe Hukushtuka Wakati Unapewa Majibu Basi Bira Shaka Ulikuwa Unajijuwa Kama Umeshaoza Ndio Maana Ulichukulia Poah.
 
Kama Wewe Hukushtuka Wakati Unapewa Majibu Basi Bira Shaka Ulikuwa Unajijuwa Kama Umeshaoza Ndio Maana Ulichukulia Poah.
Kua na maambukizi ya UKIMWI ni kuoza[emoji15]
Mkuu, ebu temea mate chini aiseeee...... omba Mungu isitokee ukapata maradhi haya.
Kumbuka ukimwi huambukizwa kwa njia nyingi tofauti na tunavyo waza ngono zembe tu
 
Watu huogopa kupima kwasababu jamii bado haija elimika vya kutosha kuhusu gonjwa hili la ukimwi. Na hii husababisha watu kua waoga kutaka kujua afya zao kwasababu moja kubwa ambayo ni ikiwa jamii itawajua kwamba wana maambukizi, watatengwa na kunyanyapaliwa
 
Kama Wewe Hukushtuka Wakati Unapewa Majibu Basi Bira Shaka Ulikuwa Unajijuwa Kama Umeshaoza Ndio Maana Ulichukulia Poah.
Duuuh ameoza???!!!! Hujafa hujaumbik ndugu no body knows tomorrow..... Napita tuuu
 
Hadithi inaonesha jamaa alishajikubali kabla hajaenda kupima..hospital alifuata taratibu tu zilizopo! Apunguze kujitapa!! Kupima na kujikubali ni jambo pana na sio kirahisi hivyo kam jamaa alivyotiririka kwenye story.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…