Kwanini watu wanaonekana kufikia hatua ya kukata tamaa na kujiua? jamii imeshindwa kuona ishara?

Kadhakan

Senior Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
126
Reaction score
201
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali za watu wanaoripotiwa kufariki kwa kujiua, huku sababu zinazotajwa zikitofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine kama msongo wa mawazo na changamoto za maisha, Afya ya akili, migogoro ya mahusiano na familia, magonjwa na changamoto za kiafya, upweke na kukosa mtu wa kuzungumza naye.

Soma pia: Kemea roho ya kujiua juu yako na watu wako wa karibu

Kwa mujibu wa shirika la Afya duniani WHO zaidi ya watu 720,000 hufariki kwa kujia duniani kila mwaka, huku vijana wakiwa miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari kubwa.

Tufanye nini ili mtu anayepitia kipindi kigumu ajisikie yuko salama kuomba msaada kabla hali haijawa mbaya zaidi?



​
 
Mkuu watu wanajiua kwa kukosa option

Hata wanapojaribu kuonyesha hisia zao na kuomba msaada, badala ya kueleweka huishia kubezwa kusimangwa na wakati mwingine kufanyiwa bullying

Wanafunguka kwa matumaini ya kupata faraja lakini wanajikuta wameumia zaidi

Dunia haina huruma kila wakati
Watu wabaya wapo wengi.lakini hilo halimaanishi kwamba watu wazuri wameisha watu wazuri wapo tuwe makini kufanya uchaguzi wa watu wa kushirikisha

Ukweli mwingine mgumu ni kwamba wengi wetu tunatembea na majeraha yetu wenyewe
Unaweza kumfuata mtu ukimweleza matatizo yako ukitarajia akutie moyo, kumbe na yeye mwenyewe anapambana na sonona ana majanga pia yeye mwenyewe anaitaji faraja

Ndiyo maana ni muhimu kujijenga ndani yako mwenyewe bila kutaka sana kushikwa mkono

Jifunze kusimama mwenyewe, kujituliza, kuvumilia na kukabiliana na changamoto bila kutegemea kila wakati mtu mwingine awe backup yako(nina ushuhuda na hili)

But ukiona mambo yamekuzidi usione aibu kuomba msaada
Mficha uchi hazai Saulaaa tu ili mradi upone
 
Jifunze kusimama mwenyewe, kujituliza, kuvumilia na kukabiliana na changamoto bila kutegemea kila wakati mtu mwingine awe backup yako.
Kwa mawazo haya ninaona kabisa safari ya u-single mother ikianza taratibu. Waoneeni huruma hao watoto mnaowaleta duniani. Huo mpango wa kulea watoto na mzazi mmoja, haukuwa mpango wa Mungu.

Watoto wa siku hizi wana tabia za ajabu ajabu kwasababu ya kukosa malezi ya wazazi wawili.
 
Ilibaki kidogo hivi 🤏 au basi

Nashauri next time ujifunze kusoma na kuelewa soma then elewa

NB: kuhusu uwezekano wa kuwa single mother sio jambo la ajabu sana
Hasa uki engege na kuzaa na mwanaume tahira
 
Ilibaki kidogo hivi 🤏 au basi

Nashauri next time ujifunze kusoma na kuelewa soma then elewa

NB: kuhusu uwezekano wa kuwa single mother sio jambo la ajabu sana
Hasa uki engege na kuzaa na mwanaume tahira
Huwa sitishwi na reaction za watu walichanganyikiwa kama wewe. Nimekusoma vizuri tu; badala ya kujibu kwa hoja unakuja na mihemko tu hapa. Usikosolewe wewe ni nani?
 
Jua Kali linachoma sana mvua hamna mfukoni huna kitu, waja mniokoea elfu Tano nipate ata maji ndo kushikana mkono hivi wadugu sio lazima nikate tamaa na ndugu zangu mpo
 
Umeongea point tupu
 
Watu wote wanadanganywa ila kujiua sio tatizo , dunia yote ni fake ni kama tunaishi kwa mazoea. Mwisho wa siku umepoteza muda tu , suala hilo lichukuliwe kama maamuzi binafsi kwani kufa ni lazima , tunaona pale Nepal wameshapoteza uhai wao bila ya kusudio .

Kufa ni jambo zuri ni wasiwasi tu kwa vile experience mpya .
 
Huwa sitishwi na reaction za watu walichanganyikiwa kama wewe. Nimekusoma vizuri tu; badala ya kujibu kwa hoja unakuja na mihemko tu hapa. Usikosolewe wewe ni nani?
Ona huyu 😅😅
Unajua tofauti ya kukosoa na kumshambulia mtu
Huwezi kujenga hoja au kukosoa kwa fact relax sio lazima uni quote mzee pita hivi

NB : sitishwi kabisa na mtu aina yako
Ila sipendelei pia ku engege na
Watu kama wewe so punguza shobo ku ni quote unless una fact
 
Kuna watu wanapitia magumu sana mpaka mtu anafikia hatua ya kujitoa uhai ameona akapumzike
 
Reactions: Lax
Kitu pekee ambacho hua nasikitika mtu akijiondoa hapa duniani kwa mambo kama hayo, watu waliomzingika kufanya kama wamesikitika
Usishangae mtu kufa kwa njaa
Na msibani kukapikwa pilau
Unafiki ni mkubwa kuliko kawaida
 
Reactions: Lax
Jua Kali linachoma sana mvua hamna mfukoni huna kitu, waja mniokoea elfu Tano nipate ata maji ndo kushikana mkono hivi wadugu sio lazima nikate tamaa na ndugu zangu mpo
Wakuu msaada
 
Kama sio Tatizo, Kwanini Wewe hujajiua mpaka muda huu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…