Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali za watu wanaoripotiwa kufariki kwa kujiua, huku sababu zinazotajwa zikitofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine kama msongo wa mawazo na changamoto za maisha, Afya ya akili, migogoro ya mahusiano na familia, magonjwa na changamoto za kiafya, upweke na kukosa mtu wa kuzungumza naye.
Soma pia:
Kemea roho ya kujiua juu yako na watu wako wa karibu
Kwa mujibu wa shirika la Afya duniani WHO zaidi ya watu 720,000 hufariki kwa kujia duniani kila mwaka, huku vijana wakiwa miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari kubwa.
Tufanye nini ili mtu anayepitia kipindi kigumu ajisikie yuko salama kuomba msaada kabla hali haijawa mbaya zaidi?
Mwenendo wa afya ya akili kwa wanajamii wakati huu.
Hili ni somo pana sana na ili kuweza kufahamu ni kwa jinsi gani au nini kifanyike katika kuhakikisha afya ya akili ya kila mwanajamii inakuwa salama. Ni vyema kufahamu ni wapi tumejikwaa ili kuparekebisha.
Ili jamii na wanajamii kuwa na afya ya akili njema mnyororo ufuatao ni baadhi ya vitu vinavyohitajika kutizamwa vyema:
1: Afya ya akili ya mama mjamzito na afya ya mama mjamzito kwa ujumla.
Ili umpate mtoto mwenye afya njema, ni vyema kutambua kwamba mama mwenye kiumbe tumboni anastahili kupata lishe bora na kukingwa dhidi ya misukosuko mikali ya maisha. Misukosuko husika inaweza kuhusisha kazi ngumu, maneno makali na yote hasi yanayoasili saikolojia yake.
Misukosuko ya maisha huchangia mtoto kutokuwa na afya njema, hii ikihusisha ukuaji na maendeleo ya mtoto.
2: Matumizi ya vilevi wakati wa ujauzito
Matumizi ya vilevi vikali kwa kiasi kikubwa wakati wa ujauzito huathiri ukuaji na maendeleo ya mtoto. Hii huathiri hali ya afya ya ubongo na afya yake ya akili kwa ujumla.
3: Malezi wakati wa utoto
Malezi ya watoto kwa sasa yameachiwa jamii zaidi kuliko wazazi wenyewe. Ingawa kuna usemi kwa sasa kuwa watoto wamebaki kuwa wa familia husika. Watoto wetu wengi wanajilea wenyewe au kulelewa na jamii. Wazazi wamekuwa hawana muda wa kuwaangalia watoto na kuwaongoza. Watoto wwtu wengi wanatumia muda mrefu kuwa sehemu ya shule kuliko familia husika. Watoto wanapelekwa mashuleni kuishi kule wakiwa wadogo sana na jukumu la malezi kubaki kwa walimu na matroni kulea kundi kubwa la vijana wetu. Matokeo yake wazazi wanakuja kukutana na vijana wenye tabia za kijamii hasi na kuanza kushangaa. Na hii pia huwapunguzia uwezo wa uimara wa kupambana na magumu/chalenji za maisha kwani wanakuwa hawajaandaliwa vyema.
4: Maisha kwa ujumla
Maisha kwa ujumla yamepandisha changamoto nyingi/kimaisha yamepandisha uhitaji wa mafanikio ya kijamii/kiuchumi. Kabla watoto hawajakomaa vyema, wanaingizwa kwenye mashindano ya kimasomo na kuziacha studi za kazi pembeni. Shule zetu zimejielekeza kwenye mashindano ya ufauru kuliko studi za kazi na ujenzi afya ya akili njema.
Baada ya mashindano na stresi za shule, mtoto huingia mtaani na kukuta maisha yanamngojea huku yameshamwekea ni kiasi gani atahitajika apambane ili kupata mafanikio. Hii ndiyo maana ni rahisi kwa kijana wa leo kuteteleka kiakiri na kiafya kirahisi kutokana na kukosa maarifa ya kuhimili misukosiko hii ya maisha.
4: Matumizi ya dawa za kulevya
Kumekuwana matumizi makubwa ya dawa za kulevya miongoni mwa jamii. Watoto au vijana ni kundi husika kwa kufahamu au kutofahamu. Kumekuwa na maelezo ya watu wanaotoa huduma za uuzaji juisi karibu na maeneo ya shule kuweka viambata vinavyowafanya watoto kupenda kutumia vinyaji husika. Ni kwa kiaai gani au ukweli kiasi gani hili ni jukumu la mamlaka husika.
5: Unyanyapaa wa jamii na wagonjwa wenyewe juu ya afya ya akili.
Suala la afya ya akili linanyanyapaliwa na wagonjwa husika, watoa huduma za afya na jamii kwa ujumla. Hii inafanya jamii kutokutambua mapema dalili za ugonjwa au kupuuza wanapozifahamu.
6: Sayansi na teknolojia
Tumekuwa na uwezo wa.kupitia taarifa zenye kuathiri afya zetu za akili bila kujua au kwa kujua. Picha za mauaji, vita au kuogofya bila kipimo au tahadhali niwanzo wa kuumiza ubongo na mwisho ni matatizo ya afya ya akili.
Ili kupata suluhu ya afya ya akili kwa ujumla ni vyema kuvunja minyororo hapo juu na kuongeza uelewa na utoaji huduma kwa watu wenye uhitaji.
Hapa ni pale tutakapotambua kuwa mimi ni wewe na wewe ni mimi, usiwe chanzo cha kutrteresha afya ya akili ya mwenzako kwa njia yoyote ile na msaidie anaehitaji huduma husika kwa mawazo, maneno au vitendo.