Hamza Nsiha
JF-Expert Member
- Jul 25, 2022
- 221
- 197
Ripoti za utafiti zinaonesha kuwa Tanzania ni nchi mojawapo ambayo inakuja kwakasi katika idadi ya watu wenye matatizo ya afya ya akili. Mpaka sasa kati ya watu wanne basi mmoja wao yupo hatarini kupata matatizo ya afya ya akili.
Pia siku chache hapo nyuma tumesikia kuhusu kulemewa kwa idadi ya wagonjwa matika hospitali ya Afya ya akili~ Milembe, kutokana na kupokea idadi kubwa ya watu wenye matatizo ya afya ya akili kuliko ilivyokawaida.
Ukweli ni kuwa hivi sasa matatizo ya afya ya akili yanahusishwa sana na mahusiano. Hususani wapenzi ambao walikuwa wakipendana sana ndio wanaongoza katika kufanyiana matukio mabaya hadi kutoana uhai.
Binafsi ninaona kwanini watu ambao wanapendana sana wasingekuwa wanaoana. La hasha ni vema ndoa zingekuwa zikifungwa na watu ambao wanapendana kiasi hii itasaidia kupunguza matarajio baina yao na wataishi kwa amani tele.
Hivi sasa mapenzi yaliyopita kiasi yamegeuka kuwa kama hali hatarishi kwa wapenzi badala ya kuwa nguzo bora ya kujenga ndoa imara.
Watu wengi wanaangukia katika misongo ya mawazo sababu ya mahusiano yanayoonekana kuwa ni mazuri kutokana na kupendana sana.
Ikumbukwe tu kuwa, wataalamu wa afya ya akili wanasisitiza kuwa ili kuondoa msongo wa mawazo(Depression) njia mojawapo kuu ni kuondoa kitu kinachokupa huo msongo wa wa mawazo (Stressor).
Je! Unaweza kumuondoa mpenzi wako ambaye unampenda sana kama njia ya kutatua msongo wako wa mawazo katika mahusiano yasiyo na furaha?