Kwanini watu wanapenda kuandika vifupishovisivyo na tija?

Kwanini watu wanapenda kuandika vifupishovisivyo na tija?

Mapondo Mapoka

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2015
Posts
269
Reaction score
121
Hii tabia binafsi siipendi hata kidogo kwani hainatija. Mfano kuandika sn badala ya sana,xkul badala school na vifupisho vingine vingi, na wewe utaongezea.

Kama msomi;uandishi huo huashiria unamapungufu makubwa.Wewe unalionaje hili?
 
wadogo zangu nishawapiga marufuku

wakiandika meseji nawaambia andika neno moja hadi jingine sasa naona wameacha hiyo tabia

maana kama ilikua wana shida na kitu na wameandika kihuni simjibu na simtimizii haja yake
 
Tija haiwezi kuwepo kwako,na hauwezi kuiona kama msj haikuhusu!
Ila kama ni mbeambea unataka ujue kila alichotumiwa mwenzio,kazi unayo.

Wahusika wakielewana safi sana! Txt ukiisoma ww huelewi,akisoma mhusika anaielwa.
Napenda sana vfpxh ktk msj.vna 6ra.
 
ni ulimbukeni wa kuigaiga kila kitu....
yani ushamba tu,,,, hi tabia sio siri inakera...
 
Tija haiwezi kuwepo kwako,na hauwezi kuiona kama msj haikuhusu!
Ila kama ni mbeambea unataka ujue kila alichotumiwa mwenzio,kazi unayo.

Wahusika wakielewana safi sana! Txt ukiisoma ww huelewi,akisoma mhusika anaielwa.
Napenda sana vfpxh ktk msj.vna 6ra.

Sawa mkuu, maisha kama sio kupanga au kuchagua basi ni uamuzi. Simamia unachokiona kua na faida kwako.
 
mantiki ya kufupisha ni kuokoa muda hii imekaa kirika zaidi Same ages kuitumia haina shidaaa but kama ww wa 70 then unachat na kijana wa 96 hapo hamtaelewana but kwa same age ina sound Goood
 
Back
Top Bottom