Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Watu wana shida kibao zisizotatulika. Watu wana matatizo mengi yaliyo juu ya uwezo wao; wanalia maisha magumu lakini hawana mlango wa kutokea. Watu wanatafuta “solution” ya shida za kifamilia, za kibiashara, kikazi, kimasomo lakini hawaoni mwanga mbele. Ukiwaambia wamuombe Mungu, anaweza kuwasaidia, wanabeza, wanacheka, wanadharau na wengine watakutukana na kudai eti Mungu hayupo, kama yupo thibitisha.
Mimi leo nathibitisha Mungu yupo, anasikia maombi, na yuko tayari kutupa haja za mioyo yetu kama alivyoahidi:
Kila mara namuomba Mungu anilinde safarini. Nimesafiri safari nyingi sana za angani, baharini na barabarani. Katika safari zote hizo Mungu ameniepusha na ajali na hatari nyingi za waziwazi. Kuna nyakati mbili tofauti, majambazi walinivamia njiani, Mungu aliniokoa na kuwasambaratisha.
Nilimuomba Mungu nipate mwenzi mzuri wa ndoa, nikapata. Sijajuta tangu tufunge naye ndoa maana tunaishi naye vizuri.
Niliwahi kukopa mamilioni ya pesa benki – mara tatu, nikamuomba Mungu aniwezeshe kulipa pesa zote na “interest” bila kuchelewa. Mungu alisikia akaniwezesha.
Niliomba nipate kazi nzuri, Mungu alisikia. Nilipata kazi yenye mshahara mnono.
Niliomba Mungu anipe ujuzi na maarifa mbalimbali, Mungu amefanya.
Kwa habari ya magonjwa, nasema kweli tupu, Mungu ameniponya magonjwa mengi kwa miujiza baada ya kumuomba.
Wachawi wameishanivamia si mara moja, lakini kwa maombi, wamepigwa na kuaibika.
Wanaosema eti Mungu hayupo, tuwasamehe tu bure, hawajui wasemalo.
Baada ya kusikia ushuhuda huo wa kweli, naamini hutapuuzia tena kumuomba Mungu.
Mathayo 7:7-12 (NEN)
“Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa kuwa kila aombaye hupewa; naye kila atafutaye hupata; na kila abishaye hufunguliwa mlango. Au ni nani miongoni mwenu ambaye mwanawe akimwomba mkate atampa jiwe? Au mwanawe akimwomba samaki atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?"