Dave official
Member
- Jul 27, 2022
- 38
- 90
Kwa aliye matured katika Imani yampasa kuamini tu
#maombi ni kwa mtu aliye katika hofu mchanga kiimani.....✍️
#maombi ni kwa mtu aliye katika hofu mchanga kiimani.....✍️
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama nilivyokujibu awali, uovu uliopo duniani ni matokeo ya dhambi iliyotendwa katika bustani ya Eden. Kuanzia wakati ule dhambi ya uuaji iliingia. Hata hivyo siku inakuja ambapo watenda dhambi wote watatupwa katika moto wa milele. Na walioishi sawasawa na mapenzi ya Mungu wataingia mbinguni, kusikokuwa na vita wala uovu wowote.Mungu huyu huyu ambaye anaruhusu vita kila kona ya Dunia?
Ili upate unayoyaomba zingatia mambo haya yafutayo:weka vigezo na mashart
Kuna vitu vya msingi unaficha ndio maana watu wengi hawana imani manake kama wewe unavyosema ndivyo wasemavyo wachungaji lakini hawasemi siri za ndani; wanaomba kwa njia gani, nini siri ya maombi yenye kujibiwa, namna gani ya kuombo ujibiwe, nk.Mungu anawapenda watoto na anasikia vibaya wanapofanyiwa uovu(Mathayo 18:6). Lakini kwa sasa, dunia hii imeathiriwa na dhambi ile ya wanadamu wa kwanza, Adam na Hawa. Uovu uliopo ni matokeo ya dhambi zetu wenyewe, sio kosa la Mungu.
Hata hivyo siku ya mwisho, Mungu atamhukumu kila atendaye uovu (Ufunuo 20:12). Hivyo hao wanaobaka watoto usifikiri wako salama wasipotubu.
Mungu hapendi uovu ndiyo maana alimtuma Yesu ili kuleta wokovu. Watu wote duniani wakiokoka, hakutakuwa na mtu wa kubaka watoto.
Kuokoka ni kufanyaje kwanza ili nisije kukubali mkataba ambao sijausomaAsante kwa kuwa wazi. Sasa hatua ya kwanza kabisa ya kujibiwa maombi ni kuwa na uhusiano mzuri na Mungu. Ukiokoka, Mungu anakuwa Baba yako na wewe unakuwa mtoto wake. Ndio maana ya andiko lile la Mt 7:7-12, kwamba Baba yetu wa mbinguni atatupa vitu vilivyo vizuri...
Ukiomba Mungu akupe mahitaji yako wakati bado unaendelea kutenda dhambi, ni vigumu kupata majibu. Mungu hamsikii mwenye dhambi. Soma Yn 9:31 (SUV). Imeandikwa hivi: "Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo."
Sala ya mwenye dhambi anayoisikia Mungu, ni sala au maombi ya toba. Kama nilivyosema, mwenye dhambi akiishatubu anakuwa mtoto wa Mungu, hapo ndipo lolote aombalo atapewa na Baba(Yn16:23).
Je, uko tayari kuokoka sasa nikuongoze sala ya toba?
Mimi siamini katika kuokoka kama mleta mada anavyosisitiza. Maana hakuna ajuaye ameokolewa hadi ile siku ya mwisho, na kama binadamu tuko prone kutenda dhambi, yaani kuanguka na kuinuka, hata Yesu alisema. Nina msusi wangu "ameokoka" lakini anaishi na mwanaume bila ndoa, sasa yeye na mimi nani mwenye unafuu kwenye eneo la uzinzi? Ni neema tu ya Mungu inatuokoa maana anazijua dhamiri zetu.Kuna vitu vya msingi unaficha ndio maana watu wengi hawana imani manake kama wewe unavyosema ndivyo wasemavyo wachungaji lakini hawasemi siri za ndani; wanaomba kwa njia gani, nini siri ya maombi yenye kujibiwa, namna gani ya kuombo ujibiwe, nk.