Kwanini Watu wema wanateseka?

Kwanini Watu wema wanateseka?

Labda wewe ni miongoni mwa watu ambao wanajitahidi sana kufanya yaliyo mema machoni pa Mungu na kusaidia jamii.

Hata hivyo pale unapopata mateso maishani labda kwanini ninateseka hata ingawa nimejitahidi kufanya yote yaliyomema!

Endapo umefikia hatua hiyo na kujiuliza maswali hayo, nakutia moyo kuwa hauko pekeyako. Na kwakweli kwa silika ya mwanadamu ya kupenda haki, kuona wanadamu wema wanateseka ni lazima kutatokea maswali kama hayo na hata zaidi labda ukatilia shaka kusudi la Mungu kutuumba au hata kuwepo kwake.

Fuatilia nami kwenye Kiambatishi
Hiyo tafsiri ya wema ni according to nani?

Unachoita wema ni shida Kwa mwingine so kama anaweza kukusulibu lazima akupelekee moto.
 
Unaweza kutenda mema ukamuudhi Mungu nikupe mfano. Kuna gari lilidumbukia kwenye maji pale kamanga mwanza. Vijana waliojitolea kwenda kuokoa walipokuja maaskari waliwatoa kwa virungu na fimbo eneo la tukio kwa maana ya kuingilia majukumu yao mamlaka ya uokozi. Yaani wao mamlaka ndo wanajua mfumo na mipango ya uokozi inavyokwenda. Tunaenda sasa kwenye maada.

Mungu ndiyo hupanga kila kitu. Hata mateso kwa watu unaowahurumia wewe anakuwa kayapanga yeye. Huenda hao watu kuteseka kwao ni adhabu ya Mungu kwa mkosa yao ya nyuma ama wazazi wao
Sasa we unapowasaidia utakuwa umepinga hukumu ya haki ya Mungu juu ya waharifu. Kwa kifupi umetorosha wafungwa wa Mungu katika gereza la Mungu na bado unataka Mungu akuongezee baraka. Hapo anachokifanya ni kukuweka na wewe gerezani kwa kosa la kutaka kutorosha wafungwa wake. Tena ikibidi wewe adhabu yako yaweza kuwa kubwa kuliko hata hao.

Hapo ndo watu wema yanapowakuta mambo mabaya. Ushauri

Acheni kutorosha wafungwa wa Mungu kwa kujifanya munahuruma sana
Huyo mungu ana roho mbaya na roho ya kichawi yaani babu zangu watende maovu kwa wakati yao eti laana yao ije inipate mimi na mungu anipe laana na adhabu mpaka vizazi vyangu vya nne, hakika huyo mungu ni zaidi ya mchawi.
 
Labda wewe ni miongoni mwa watu ambao wanajitahidi sana kufanya yaliyo mema machoni pa Mungu na kusaidia jamii.

Hata hivyo pale unapopata mateso maishani labda kwanini ninateseka hata ingawa nimejitahidi kufanya yote yaliyomema!

Endapo umefikia hatua hiyo na kujiuliza maswali hayo, nakutia moyo kuwa hauko pekeyako. Na kwakweli kwa silika ya mwanadamu ya kupenda haki, kuona wanadamu wema wanateseka ni lazima kutatokea maswali kama hayo na hata zaidi labda ukatilia shaka kusudi la Mungu kutuumba au hata kuwepo kwake.

Fuatilia nami kwenye Kiambatishi
Labda mawazo ya Mungu si kama ya Mwanadamu
 
Back
Top Bottom