TGInnocent
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 1,088
- 582
- Thread starter
-
- #21
solution
1/2×(3×10) +(5×5)=40
~=40 sm square
Kilaza
Pole Jodoki, lakini bado tunapaswa tufikirie ni jinsi gani tufanye vijana wetu walipende somo hili bila kujali vikwazo kama ulichokutana nacho. Kumbuka hata maisha nayo huwa hostile sana lakini hayatuzuii kupambana nayo. Wakati mwingine kejeri, viboko, kubezwa zaweza kuwa nguvu za kutuchochea kufanya vizuri.
mmmh!! hisabati tena!!! mie niliziachia la7 and i was good on it, ila kufika sec miezi mi4 hakuna mwl wa hesabu, mwl kupatikana akawa anaongea na ubao anaandika alafu anasoma alichoandika, ukiongezea na kiinglish tena mara jumlisha kawa plus/addition nk. mweeee mtihani kutoka nikapata 30 nilitandikwa viboko havina idadi, yaani mzuka wa hisabati ukaishia hapohapo. ukiniuliza mada zilizofuata hata sijui
Wadau msingi ndiyo kila kitu
Walimu wa msingi wana jukumu kubwa la kuhakikisha hisabat linakuwa somo pendwa
daah wachanijue kutoa na kujumlisha maana kama mtu amefeli kidato cha nne ile mihesabu itamsahidia nini kwamfano. matrixs.. sijui log kama sio wehu nin?... Hesabu ni kipaji tu wengine tumenyimwa bwana dada kapata hesabu A n history ana F
Mathematics ilinishinda senior two yani mpaka leo nikiona sipendi labda hizi kujumlisha, zidisha, gawanya, toa ndo naziweza
mmh! mie mwl wangu wa msingi alijitahidi sana kwakweli na kwa wakati ule nilikuwa cpati chini ya 47/50, shida ikaja sekondari ndipo mambo yalipoharibikia
ukishajua +, -, * Na / inatosha.
Kuku wa kienyeji hizo ni kama kujua a, e, i, o, u hazitoshi kutengeneza sentensi lazima uzijue pia a, b, c, ... z. Kuhesabu ni tofauti sana na hisabati. Tupe mfano wa shughuli zako tuangalie kama zinaweza kukwepa matumizi ya hisabati.
Atoto unashauri nini kwa wasichana ambao wako vizuri katika hisabati wakiwa primary watakapofaulu kwenda sekondari na kukutana na yaliyo kusibu