Kwanini watu wengi wanapenda kusifiwa na sio kuambiwa ukweli?

Kwanini watu wengi wanapenda kusifiwa na sio kuambiwa ukweli?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Salama Ijumaa hii?

Kusifiwa ni jambo zuri, hasa ukipewa sifa ikiwa umefanya kitu kizuri. Inakupa hamasa ya kufanya vizuri zaidi. Shida inakuja ukiambiwa kinyume. Yaani mtu akikuchana ukweli unakasirika, unafura na kumuona tu hafai.

Tena ukiambiwa ukweli na mtu aliyekuwa anakusifia kila siku ndio kabisa unaumia na kuona kama dunia imeisha.

Kulikuwa na member humu anamwaga like kwenye kila uzi anaokutana nao, jamaa hadi akawa maarufu, halafu akaja mwamba ambae alikuwa anaponda na kudislike kila uzi na comment anayokutana nayo, palikuwa pamoto humu kila mtu akilalamika.

Viongozi serikalini kila siku tunaona wakisifiwa wanatoa mpaka vyeo kama sadaka, ila kinyume chake wakiambiwa kweli virungu vinatembea, mara watu wanakamatwa na kupotea, yaani tafrani.

Hii inaonesha ni jinsi gani watu wanapenda kusifiwa na kupambwa.

Kama ukweli ni mzuri kwanini watu wengi wasiupende na kufurahia kusifiwa hata kama ni uongo?
 
Watu wengi huwa wanaamini wao,yeye Ni bora (extra ordinary) sasa unapomwambia madhaifu yake you prove him wrong unam disappoint

And that is how we created tonatofautiana to reaction pindi tunapokosolewa baadhi wanamezea na kubadilika baadhi unakua uadui
 
SWALI: Kwanini watu wengi wanapenda kusifiwa na sio kuambiwa ukweli?
JIBU: KWA SABABU NI WANA CCM

Mwisho wa Uzi.
 
Sometimes hatuko sure na maamuzi..
Tukisifiwa ina tupa imani tuko sahihi..
Sometimes tunajua kabisa maamuzi sio sahihi...lakini hatuna namna ingine
So tukipondwa tu..tunakasirika Kwa sababu hatutaki kukumbushwa kuwa maamuzi sio sahihi...tunajua na Yana tuumiza..
 
Back
Top Bottom