Kwanini watumishi wa Umma wawe na Masters na PhD?

Nimefuatilia hoja za viongozi wengi wa Umma wenye PhD na Masters, kila wanaposimama kuzungumzia mstakabali wa nchi yetu wamekuwa wepesi sana KUTUDANGANYA.

Matumizi ya elimu za wasomi ambao ndio viongozi waandamizi wa Taifa letu hayaendani kabisa na kile wanachokichangia kwa Taifa.

Msemaji wa serikali ana PHd ila sikiliza hoja zake katika vipindi na maeneo mbalimbali utagundua lipo tatizo la kusema ukweli hapa nchini na tatizo linachangiwa na wasomi.

Msikilize Mbobezi wa sheria, Mzee wa Mambo ya nje anapozungumza kuhusu nchi yetu utagundua lipo gonjwa la uongo ndani yetu. Waziri wa Mambo ya nje alituaminisha sisi ni matajiri na kuwaita matajiri MABEBERU huku akijua tunao mabalozi nje wanaotuombea tupate misaada na wahisani, ni kulewa UONGO wa kisomi.

Nenda kutana na mtumishi wa Umma mwenye master's na Phd zungumza naye japo kwa dakika kadhaa unagundua wazi hata kile anachokifanya hakijui.

Najiuliza kwanini tunadhani tunahitaji wasomi wakubwa kuingoza sekta ya umma hapa Tanzania?
Ni Nyerere ndiye aliwabatiza wazungu hasa wa magharibi jina hilo na so Prof Kabudi. Muombe radhi maana umemsingizia.
 
tatizo la kusema ukweli hapa nchini
hapondio shida nilipo hii nchi si wasomi tu viongozi wa uongo ni wanasiasa wakawaambukiza watendaji (wasomi) na sasa mtaani hadi kwenye mafamilia tunaishi kwa uongouongo ni hatari sanaaa.
 
Kuna PhD mwingine huku jana kawadanganya Wananchi Wanyonge eti Tanzania itakua Nchi ya kwanza Afrika kuendesha Treni ya Umeme!!
Hahaha mwalimu upo??? Ivi siku ukipata kibarua sema fedha sec. Wakakupa nyumba/ allowance, transport na mshahara mnono. Usiende ati hutakuwa mzalendo?
Uzalendo wa kununua maghorofa kwa ml 6 hull dodoma na kagawa nyumba za umma kwa kina kajala wa kebys?
 
Ninavyoelewa mimi ma- professor wengi wa nchi za wenzetu huwa kwenye academic institutions wakifundisha na kuendelea kufanya research mbali mbali ambazo siku moja zitamuwezesha kushinda hata Nobel Prize. Vile vile huandika vitabu na publications mbali mbali kama njia moja wapo ya kujiingizia kipato na vile vile kuwa kama visiting lecturers kwenye university nyingine.

Hapa kwetu ni different story. Wengi wameingia kwenye siasa na kuzitupa academic credentials zao kapuni na kuwaacha watoto wetu vyuoni wakikosa hata wahadhiri wa kuwafundisha.

Ningependa kuona ma- professor wetu kwa mfano wa Math, basi anakuwa na hata you tube channel fulani hivi ya kuwasaidia vijana wetu kulielewa na kulipenda somo ambalo mpaka sasa ni kizungumkuti kwao. Tumeliona kwa kwa ma - professor wa nchi za ughaibuni.

To his credit, Nampongeza sana Professor Ngowi wa pale Mzumbe ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuwaelimisha wananchi katika masuala ya kiuchimi na budget kwenye media mbalimbali. Hivyo ameitendea haki jamii na na fani yake ya uchumi kwa ujumla.
Well said mkuu..
 
sio kweli mkuu, labda kuna jambo moja hulielewi mkuu. Naomba nianze nawewe nipe maana ya masters na PhD. Na je hizo masters na PhD wanaomea nini? Je wasomea kuongea kwenye majukwaa au kuhutubia watu? Na je ulishawahi kuwauliza kwenye hizo PhD na masters wanasomeaga nini? Mwisho usilaum laum Kabla ya kufanya evaluation. Acha tena Acha kuwafokea zaidi utabakia kuwa mbumbu tu mpaka mwisho.
[emoji23] [emoji23] Jiwe limekuangukia utosini nini?

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Tunahitaji wasomi wakubwa kwa sababu mifumo yetu yote ni ya kisomi kuanzia mifumo ya HR,Finance na Public Service yote inahitaji wasomi hata junior staff wa Public Service wanatakiwa kuwa wasomi wazuri.

Hatuwezi kuweka ngumbalu waongoze Public Service. Ngumbalu nikimpa mfumo wa SPSS,EDMS,TANSIC nk ataiwezea wapi!!!

Ubovu wa wasomi wachache kwenye PS usi qualify kwamba hatuhitaji wasomi wazuri kwenye utumishi

Hiyo haipo
China imeendelea nje ya mfumo wa PhD, hawajawahi kuwa na Rais Dr. au Profesa.
 
Kwa taarifa yako uchina ina formal education ya kutosha ndio maana viwanda vya mass production ya technological apparatuses vinasimikwa uchina kwa sababu population ya wenye akili kufanya kama cheap labour ipo. Sasa huwezi kufananisha uwezo wa an ordinary Chinese na hawa ngumbalu wetu wanaoshinda kuongea ngono tu kwenye social media. Taasisi imara iwe ya umma au private inahitaji wasomi wazuri ktk ngazi zote kuanzia seniority positions hadi zile za chini...

Tusipotoshe ukweli nje ya formal education mtu hawezi kuwa na uwezo ila utundu, kwa hiyo hatuhitaji watundu bali tunahitaji wasomi wenye ubunifu na uzalendo.

Elimu ni muhimu saaanaaa
 
K
Nimefuatilia hoja za viongozi wengi wa Umma wenye PhD na Masters, kila wanaposimama kuzungumzia mstakabali wa nchi yetu wamekuwa wepesi sana KUTUDANGANYA.

Matumizi ya elimu za wasomi ambao ndio viongozi waandamizi wa Taifa letu hayaendani kabisa na kile wanachokichangia kwa Taifa.

Msemaji wa serikali ana PHd ila sikiliza hoja zake katika vipindi na maeneo mbalimbali utagundua lipo tatizo la kusema ukweli hapa nchini na tatizo linachangiwa na wasomi.

Msikilize Mbobezi wa sheria, Mzee wa Mambo ya nje anapozungumza kuhusu nchi yetu utagundua lipo gonjwa la uongo ndani yetu. Waziri wa Mambo ya nje alituaminisha sisi ni matajiri na kuwaita matajiri MABEBERU huku akijua tunao mabalozi nje wanaotuombea tupate misaada na wahisani, ni kulewa UONGO wa kisomi.

Nenda kutana na mtumishi wa Umma mwenye master's na Phd zungumza naye japo kwa dakika kadhaa unagundua wazi hata kile anachokifanya hakijui.

Najiuliza kwanini tunadhani tunahitaji wasomi wakubwa kuingoza sekta ya umma hapa T
Ni kweli usemayo. Nina mashaka ama na mfumo wa elimu au njaa inatafuna akili za wasomi wa nchi hii!!

Mbaya zaidi, jiwe anatumia wasomi kuharibu mambo ya nchi hii!! Wasomi wamekuwa wasaliti!

Niliwahi kuandika uzi fulani hivi kuwa Tanzania haiwezi kukombolewa na wasomi kutoka katika siasa chafu!!
 
Kwa taarifa yako uchina ina formal education ya kutosha ndio maana viwanda vya mass production ya technological apparatuses vinasimikwa uchina kwa sababu population ya wenye akili kufanya kama cheap labour ipo. Sasa huwezi kufananisha uwezo wa an ordinary Chinese na hawa ngumbalu wetu wanaoshinda kuongea ngono tu kwenye social media. Taasisi imara iwe ya umma au private inahitaji wasomi wazuri ktk ngazi zote kuanzia seniority positions hadi zile za chini...

Tusipotoshe ukweli nje ya formal education mtu hawezi kuwa na uwezo ila utundu, kwa hiyo hatuhitaji watundu bali tunahitaji wasomi wenye ubunifu na uzalendo.

Elimu ni muhimu saaanaaa
Formal na informal ni ipi na ipi, viwango vyake vya kimataifa ni vipi? Nani amekupotosha? Nimesema China INA mfumo wake wa elimu, kubali kataa itabaki kuwa hivyo, ukija na cheti chako toka China utapata jibu.
Elimu yetu si formal uingereza lakini kwetu ni formal, huo ndiyo mpangilio wa nchi husika.
 
Hoja ya msingi hapa ni ikiwa upo umuhimu wa wasomi kwenye public sector huko kwenye elimu umeamua tu kwenda mwenyewe. Msimamo wangu kulingana na mada ni kwamba tunawahitaji mnoo wasomi kwenye sekta ya umma hata binafsi ikiwa nia ya kuendelea tunayo
 
Ninavyoelewa mimi ma- professor wengi wa nchi za wenzetu huwa kwenye academic institutions wakifundisha na kuendelea kufanya research mbali mbali ambazo siku moja zitamuwezesha kushinda hata Nobel Prize. Vile vile huandika vitabu na publications mbali mbali kama njia moja wapo ya kujiingizia kipato na vile vile kuwa kama visiting lecturers kwenye university nyingine.

Hapa kwetu ni different story. Wengi wameingia kwenye siasa na kuzitupa academic credentials zao kapuni na kuwaacha watoto wetu vyuoni wakikosa hata wahadhiri wa kuwafundisha.

Ningependa kuona ma- professor wetu kwa mfano wa Math, basi anakuwa na hata you tube channel fulani hivi ya kuwasaidia vijana wetu kulielewa na kulipenda somo ambalo mpaka sasa ni kizungumkuti kwao. Tumeliona kwa kwa ma - professor wa nchi za ughaibuni.

To his credit, Nampongeza sana Professor Ngowi wa pale Mzumbe ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuwaelimisha wananchi katika masuala ya kiuchimi na budget kwenye media mbalimbali. Hivyo ameitendea haki jamii na na fani yake ya uchumi kwa ujumla.

Hebu karibu hapa: ***** Open Discussion Forums Integrated Software and Technologies for Teaching and Research na wewe utoe mchango wako katika sekta ya elimu. Kwa nini unasubiri watu wenye PhD?
 
Back
Top Bottom