Hatari sana, kuna mahala watu wanapaswa kuchimbua uhalisia na kuja na majibu.
Bado huwa natafakari, inamaana hawa waislamu ni wajinga kiasi hiki na kuamua kuuaua tu watu hovyohovyo bila sababu?
Kwanini hivi vikundi vipo? Hamas, Boko Haram, IS, ALQEDA nk?..
IS chimbuko lake ni IRAQ, Sadaam akiwa Rais wa Iraq hakukuwepo IS wala Alqaeda Iraq na influence ya hayo makundi hapo middle east, toka USA wameingia IRAQ na kumuua Sadaam, IRAQ ikawa safe heaven ya hayo makundi.
SYRIA hakukuwepo na hayo makundi wala influence yake, watu waliishi kwa amani na raha, pale USA walipokuja na operation ya kijinga kumuondoa Assad pale Syria shida ndio ikaanzia hapo na mpaka leo Syria kumekuwa na dominance ya hayo makundi.
LIBYA ilikuwa shwali kabisa na watu wakiishi kwa raha, shida ilianzia pale USA walipomtoa Ghadafi, mpaka leo kumekuwa na influence kubwa ya hayo makundi.
1947 lilipoanzishwa Taifa la Israel Mashariki ya kati ndipo pia vuguvugu ya haya makundi lilipoanza, na mengi sana yalianzia pale Lebanon kwa minajili yakuwasaidia Palestina kupigania ardhi yao na kuifanya iwe huru, operationa ya makundi haya yaliendelea na kupambana kwa namna nyingi ikiwepo utekaji wa ndege, kujitoa muhanga nk. Hali hii iliifanya USA kuendesha operation nyingi mashariki ya kati ili kuilinda Israeli ikiwepo kusimika hata viongozi kwa maslahi ya USA, ISRAEL nk, mfano Sadaam Hussein Iraq na hata kumlinda Mfalme Shah wa Iran dhidi ya Ayatolla nk. Hali hii iliibua vikundi kadha wa kadha kupambana na USA kwenye agenda zake za siri nk.
Maelezo ni marefu yanayohitaji muda na utulivu, kuanzia Crusade war, dollar ya rumi, operation za roman catholic, dollar ya Ottoman, mazayuni na mambo yao, USA+alliencies wake na mambo yao nk... kwa pamoja haya yote yamezaa Hamas, Hizzbollah, IS, Boko Harama, AlAqsa, Muslim brother's nk..