Kwanini waumini Wa zama hizi wanaogopa Sana Teknilojia?

Kwanini waumini Wa zama hizi wanaogopa Sana Teknilojia?

Mkuu naomba ufafanuzi hapo kwenye "Carrier Mother ".... Natamani kujua unamaanisha nini... kwa manufaa ya wengine pia. Asante
Hii ni pale Ambapo huna uwezo wa kuzaa then unamlipa mwanamke pesa ndefu ili akubebee mimba. Iwe kwa kununua sperms kutoka sperm bank ama kwa mbegu na yai lako ama mimba yako vinatolewa na kupandikizwa kwa mwanamke mwingine.

Mfano ni jinsi watoto wa Michale Jackson walivyopatikana wakina Prince na Paris.

Kwenye old times, yaani biblical times. Hii inaweza fanana kidogo na jinsi Sarai mke wa Abramu alivyotaka kupata mrithi wake kupitia Mwanamke Mtumwa aitwae Hagari. Ambapo Ishmaeli alizaliwa ili kua mrithi wa Sarai aliekua mgumba. Hapa hagari ali play kama carrier mother. Though hakubeba Yai la uzazi la Sarah. Na Mwenyezi Mungu akabariki mchakato wote

.
 
Pengine alimaanisha 'foster mother'
Foster huyu ni tofauti kidogo huyu ananyonyesha na kulea mtoto wa mwingine kwasababu mbalimbali hata za kiafya ama mama kafariki nk. Akiwa na lengo la kulinda uhai wa mtoto.
lakini anakua hakubeba mimba ya huyo mtoto.

Carrier mother ama Gestational carrier anakua alibeba ujauzito wa Wengine. Yeye anatumika kama medium tu ya kutunza uzazi mpaka mtoto azaliwe.
 
Back
Top Bottom