Kwanini Wayne Rooney hakutwaa Ballon D'or?

Mchochezi

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
10,962
Reaction score
7,830
Kwa miaka kumi na tano iliyopita, Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya England ambaye kwasasa anakipiga katika klabu ya Everton alikuwa katika fomu ya juu sana.

Ni katika kipindi hiko, Wayne Rooney au Pele Mweupe kwa jina la utani, alitwaa kila taji katika ngazi ya klabu.

Wayne Rooney ametwaa mataji matano ya EPL.

Ameteaa Uefa Champions League, Uefa Europa League, F.A cup, Klabu Bingwa ya Dunia, bila kusahau Carling cup na Ngao ya Hisani.

Hiyo inamfanya kuwa Muingereza mmoja kati ya Waingereza wawili kutwaa kila taji kwa ngazi ya klabu.

Dunia ya mashabiki wa soka haikuwahi kumtazama Rooney kwa umakini na kumpa sifa zake. Mimi naamini katika miaka 10 mpaka 15 iliyopita Rooney alistahili kutwaa mchezaji bora wa Dunia walau mara mbili hivi.

Je ni kwanini FIFA walimnyima Rooney tuzo ya mchezaji bora wa Dunia akiwa katika ubora wake?
 
Kabla hujawalaumu FIFA jiulize kwanza ni akina nani wanapiga kura za mchezaji bora wa dunia?
 
Siasa ya mchezo wa soka; wenye maamuzi nani awe nani kwenye soccer ni wale wenye maslahi makubwa mapana na ya moja kwa moja na mchezo huo.

Angalia, CR7 na LaPulga, wooote wanaaminishwa kwenye soccer kwa sasa ni hawa wawili tu!

Xavi alishangaa alipoona hakupewa yeye tuzo ile ila akasema kwakuwa amepewa teammate, haina shida!

Hata hivyo, mchezaji bora wa dunia anatoka kwenye ligi maarufu na zenye hela tu..
 
kwahiyo ligi ya epl haina hela?
 
kwenye hiyo era kulikuwa na kina xavi, cr7, lionel, iniesta,kaka n.k ambao kwa hali ya kawaida ni uwendawazimu rooney kupewa hiyo tuzo.... mwaka ambao utd ilitamba sana sana na kuchukua mataji yote ni 2008, hapo alikuwepo team mate wake cr7 akaichukua hiyo tuzo.... baada ya hapo ni mwaka gan utd wameweza kuchukua tuzo nyingi kwa season moja ? jibu hakuna... naposema tuzo kubwa namaanisha UEFA na ubingwa wa ligi mfano EPL. Sio timu ishinde FA na CARLING CUP alafu utegemee itoe mchezaji wa kubeba ballon d or.
 
Siasa za mpira zina mambo yake sishangai uyo Rooney maana Xavi na Iniesta mpaka wanafika mwisho Ballon D'or wameiona kwa Messi kwa kua Dunia ya soka iliwakataa bila sababu.
 
Siasa za mpira zina mambo yake sishangai uyo Rooney maana Xavi na Iniesta mpaka wanafika mwisho Ballon D'or wameiona kwa Messi kwa kua Dunia ya soka iliwakataa bila sababu.
fact
 
Mmmh hembu naomba nitajie ni mwaka gani unahisi Rooney ali deserve Balon d'or?Halafu uangalie mwaka huo kachukua nani?na jee ni kweli ana deserve au kapendelewa?Msimu ambao atleast Rooney angeclaim kuchukua ni 2007/08 ambao ndio walibeba UCL pale Moscow but Cristiano Ronaldo was the star performer without a doubt!!Atleast mtu akinambia Iniesta au Xavi au Sneijder au hata Ribery (2013) wamedhulumiwa apo kidogo ningekuelewa lakini Rooney aargh hivi kashawahi kushinda hata PFA players player of the year award na kama kashinda itakua moja tuu
 

Pole sana naona waingereza wamekulisha pumba zao na wewe ukaziamini hahaha Kuna wachezaji bora zaid katika kipindi chake na hawakupata balondoir i.e. Henry, Drogba,
 
Unanikumbusha wiz wa wazi waliomfanyia xavi,iniesta,sneider.
Hakuna anaepinga ubora wa rooney na msim wa yeye angalau kupata ndio alibeba ronaldo na alistaili 2008.
Lkn hao jamaa nashangaa akina iniesta cjui waliwakosea nn yaan hata moja wagawane hakuna?..daah
Akina neymar watakuja kuchukua di'or nyepesi sana huko mbeleni.
 
Unaposema miaka 10 -15 iliyopita unaanza kuchukua kipindI PROPHET GAUCHO yupo, akaacha Maswahaba wake Kaka, CR7, Messi ambao nao wanaacha uzao kwa Neymar na Dyabala ili kuja kukamilisha utakatifu ktk soka. Miaka hiyo unayosema ww ROONEY hata kupiga kengere kanisani au au kubeba mikate ya Sacrament alikua apewi.
 
Pole sana naona waingereza wamekulisha pumba zao na wewe ukaziamini hahaha Kuna wachezaji bora zaid katika kipindi chake na hawakupata balondoir i.e. Henry, Drogba,
Drogba kamzidi nini Rooney?
 
Kwa kua tuzo ni moja basi anabeba mmoja..

Ila imejaa upendeleo sana...
Xavi,
Iniesta
Sneidjer
Ribery
Nuer
Kna kipindi walstahili kabsa..

Kesi ya Wazza ni timu yake kumpa majukumu mazto, hii ilimpumguzia ubora wa kufocus na ufungaji pekee ktu ambacho ndio knatazamwa sana kwa sasa..
No Doubt msimu wa 2009/10
Wazza alikua fomu sana kias alkua mshambuliaji hatari kabsa kwa kipindi kile...
Sometime bahati pia.. Esp. Wesley Sneidjer 2010
 
Uko sawia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…