Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Suala la DP World ya Waarabu wa Dubai kuwekeza katika bandari zetu linadaiwa kuwa na faida nyingi sana kwetu kama Taifa.
Inadaiwa mkataba utachagiza na kuchochea ukuaji wa sekta nyingine za kiuchumi (multiple effect) zikiwemo kilimo, utalii, viwanda, mifugo, uvuvi, biashara na usafirishaji na hivyo kuboresha ustawi wa Watanzania kwa ujumla.
Pia inadaiwa kuwa mkataba huu utaweka mifumo ya kisasa ya TEHAMA inayohitajika na TPA.
Zaidi ya hapo mkataba huu unadaiwa utawezesha huduma za TPA kuwa bora na zenye ufanisi wa kuridhisha na zilizo wazi kwa Watanzania na wadau, katika uendeshaji wa bandari za Tanzania.
Na kadhalika...
Mkataba huu pamoja na kupingwa na idadi kubwa ya Watangayika, unaonekana kuungwa mkono karibu na asilimia 100% ya Wazanzibar
Swali: Kwa nini hakuna Mzanzibari hata moja anayelalamikia kitendo cha Mkataba huu wa DP World ya Waarabu wa Dubai kuwatenga wasinufaike na wao?