Kwanini wazawa utajiri wetu ni wa kawaida?

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
704
Reaction score
2,435
Nimejiuliza nimekosa majibu, 2015 alikuja mhindi mmoja nyumbani akiomba nimpatie gari abebe vyuma chakavu from Jombe to Kibaha , since then amekuwa kama mshikaji bado nampakilia sana vyuma, kinachonishangaza amekusanya mtaji mkubwa kwa miaka michache, pesa aliyonayo ni kubwa sana, wakati najitafuta yeye kawa na mtaji mkubwa, nikitazama background yake dah ni ngumu kuliko mimi, najiuliza ni mbinu gani wenzetu wanazo watu wa asili ya asia.
 

Wahindi wana vikundi vyao vidogo vidogo wanasaidiana mitaji kwa zamu
 
AKILI zina mushkeli!

Mabadiliko yoyote yale aidha yawe chanya au hasi, lazima huwa yanaanzia KICHWANI (AKILI).
 
najiuliza ni mbinu gani wenzetu wanazo watu wa asili ya asia.
Wana Consistency na discipline kwenye kila wanachofanya.

Wana Mentality/Mindset za kitajiri. hawafanyi vitu ili uwaone wana Pesa(Show offs), hii inafanya matumizi ya Pesa zao yanatumia kwenye vitu vya Msingi na muhimu sana.

Mwisho, Jamii yao wanapeana Support kwenye issues za msingi kuliko za Kijinga. Mf, Ukianzisha biashara wahindi wenzako ndio wanakuwa wateja wakubwa.
 
Wanaroga Mzee wangu nenda Zanzibar au Pangani ukajisafishe, baada ya hapo endelea na kupiga mzigo miaka sio mingi mtakua level moja au utamzidi kabisa ingawa Mimi siamini sana hizo Mambo maana muamuzi wa yote ni Mungu
 
Majungu,ushirikina ,fitina,kijicho na ujinga uliokithiri.
 
Waswahili hatuna utamaduni wa kusaidiana

Wenzetu wanasaidiana sanaa

Waswahili wanaona mpaka uajiriwe ndo umeyapatia maisha
Tuna safari ndefu sana akili za vizazi vyetu zina fikra za utumwa bado ilhali tumeshatoka huko..
Utumwa ulituathiri sana..
 
Pesa ni roho
Pesa ni suala la kiroho kwanza kabla halijawa la kimwili
Pesa Ina mfumo wake(mifumo yake)
usifikiri ni issue ya kutafuta tu ,Kila mtafutaji angekuwa tajiri....

Behind wanajua wanachofanya ila hakuna anaeweza kukwambia!
 
Ushauri mdogo kutoka kwangu ni kuwa jaribu kufanya mambo yako kisirisiri, tuache showoff tutatimiza malengo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…