Kwanini wazazi wengine wanachagua koo na makabila ya kuoa?

Kwanini wazazi wengine wanachagua koo na makabila ya kuoa?

Sumbalawinyo

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2009
Posts
1,282
Reaction score
248
Ukiwauliza, baba kwanini nisimuoe huyu binti, utasikia akisema, sisi hatuoi ukoo au kabila analotoka huyo msichana.
Ukiuliza kwa nini, unajibiwa eti ni mila.
 
mimi ni lema siwezi oa kwa wakina muro,massawe,malya,nkya,swai eti wazazi wanasema wao ni maskini,,du!
 
Nafikiri sababu za msingi ni kua hua wanajuana kwa tabia
wanajua kuna tabia ambazo si nzuri katika ukoo huo hivyo hujaribu
kuepusha ili walau hata watoto watao zaliwe wasiwe subjected kwenye
tabia hizo... mfano uvivu, uchawi, nuksi, n.k
 
huyo baba yako ni kilaza.
Kuna koo zenye magonjwa ya kurithi na pia makabila na koo nyingine huwa na matabia ya ajabu ajabu lama vile ujambazi, ufuska, uchawi, nk
 
mimi ni lema siwezi oa kwa wakina muro,massawe,malya,nkya,swai eti wazazi wanasema wao ni maskini,,du!

nyindaroo lema woomi kumbe sisi akina lema tusiguse huko na kwa mushi tuoe
 
mimi ni lema siwezi oa kwa wakina muro,massawe,malya,nkya,swai eti wazazi wanasema wao ni maskini,,du!

Swai mbona mambo safi?!Lema ni balaa maana nawajua kadhaa kichwani hazijakaa sawa!!

Nwy yote ni ubaguzi wa kizamani!!!
 
na baba au mama akishakwambia usioe kwenye koo flani usijaribu kupinda shingo utajutia tu nimeona mengi,wazazi wanajua mengi na wanawatakia mema watoto wao,hata akisema ukoo ni masikini sio mbaya kwa sababu sio mpango wa Mungu mtu kuwa masikini wachaga wako sahii.piga mzigo uone kama umasikini utakuwepo.
 
Hakika umenena la maaana
 
Si kwamba wazazi wanakuwa sahihi, ila inabidi tu tuwe watii. Nilivyokuja kugundua wazazi wanawatia mikosi watoto wao. Kama umekatazwa kuoa/olewa na mtu fulani wewe ukapuuza basi mara nyingi ndoa yenu inakuwa na mikosi. Unakuta mara watu hawapati watoto. Mara watoto wanakufa. Yaani roho za wazazi kama hazijaridhia huleta nuksi siku za usoni.

I have seen many couples ambazo zina matatizo ya kufa mtu ukichunguza wazazi walikuwa hawataki watoto waoane. Siamini supernatural power lakini haya mambo yapo. Si uchawi ila ni kama laana.
 
Mi kabila langu zamani ni kama zimejigawa kwenye koo tofauti,na kila jina la koo lina tabia yake,kuna koo ambazo zina historia kuwa ni wachawi na waganga wa kienyeji,kuna koo lingine wanatabia za kupiga wake zao au mwanamke anakuwa na role kubwa za kulinda na kukaa na familia,but kuna koo zingine hawana hayo mambo kihistoria kwa hiyo lazima mzazi kuangalia upande ambao mwanae/binti yake anapata manufaa au kumjali.
 
Kuheshimu wazazi ni moja ya amri za Mungu na lenye ahadi ya malipo yake hapahapa duniani. Mzazi akikukataza kitu hata kama ni cha muhimu na unanona baba kaenda kushoto hupaswi kukataa kama unamkatalia mshikaji wako, kuna roho ya Mungu kabeba huyo.

Hapo hakuna uchawi, ila baraka na laana alizopewa na Mungu ndo hutesa. Cha muhimu ukiona mzazi anakukatalia kumuoa binti au kuolewa na mtu, mwambie akuelewe ili aridhie uende, siyo kulazimisha bila kuibadilisha nafsi yake, lazima utalaaniwa tu, mpaka utubu kwake.
 
nadhani kutiokana na personal experience. kama walivyosema wengine, ni kabila na mengine. Lakini hata mimi, kuna badhai ya familia ninazozijua kwa undani, kama mtoto wao atakuja kuoa kwangu sitakubali kabisa!
 
Hamna mzazi anaemtakia mwanae shari ni bora ukasikia nini anakuambia ni bora umsikize na kweli kuna koo zingine sio kwa wale wahaya na wanyambo kuna ukoo mmoja unaitwa (abasingo) yaan we ukioa au kuolewa na msingo huwa ni mabalaa matupu iliwai kumtokea shangazi yang.
 
Hao wazazi wako waongo kwa taarifa yako kina nkya sio maskini hata kidogo kuanzia kimwili mpaka kiroho!
 
Back
Top Bottom