KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,147
Katika nchi zilizoendelea kuna nafasi za masomi mbali mbali wanazozitoa kwa ajili ya nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania,mimi nipo hapa Havard university nabeba box lakini kuna kitu kimoja ambacho hata sikielewi,hivi ni utaratibu gani huko nyumbani unatumika kuwapata wanafunzi wa kuja kuchukua nafasi hizo?Nauliza hivi kutokana na kushuhudia asilimia kubwa ya "wanafunzi"wanaokuja hapa kuwa ni wazee hasa viongozi..mfano alikuja hapa bwana mkubwa sumaye baada ya kutoka kwenye uwaziri mkuu huko nyumbani baadae akaja bwana Amani na familia yake,najiuliza hawa wazee wanaweza kuwa na mchango gani zaidi kwa taifa mpaka wakapewa nafasi hizo ambazo katika hali ya kawaida tulitegemea kuwaona vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa,kwanini nafasi hizo wasipewe vijana au vijana huko nyumbani wote wameelimika na hawahitaji tena nafasi kama hizo?