wazungu hawana roho mbaya na chuki?
Wazungu hawana roho mbaya mkuu..,,wala chuki,,
Mzungu ni kiumbe pekee ambaye anaweza akapanga jambo na kuwaeleza wengine,,
Mfano anataka kusafiri,
Anataka kufanya chochote cha maendeleo ,,
Atakisema hata kabla ya mwaka mzima kufika..wakati huku kwetu Africa mambo ya maendeleo mfano kujenga,,unataka kusafiri ng'ambo nk mtu anafanya siri kuogopa roho mbaya za kichawi..
Mzungu atakusaidia sana ktk kufanya jambo la maendeleo,,wakati mwafrika ukimtajia jambo la wewe kuendelea basi elewa hutofanikiwa kwa kuwategemea wao kukusaidia,..
Mfano...pengine unahitaji msaada wa kifedha ili jambo lako liende,,unaweza kumfata jamaa au ndugu kabisa ambaye uwezo wa kukusaidia anao lakini akishajuwa unahitaji ili upige hatua ktk maisha ,,kusaidiwa ni ngumu sana,,tofauti na mtu mweupe..
Mzungu hukusukuma juu uzidi kupaa wakati mwafrika atakukandamiza uzidi kushindwa..