Kwanini Website ya wizara ya elimu Haipo hewani?

Kwanini Website ya wizara ya elimu Haipo hewani?

kwa hayo majina yana wingi kiasi gani hadi yafunge tovuti?
 
This account has been suspended.

Either the domain has been overused, or the reseller ran out of resources.

or has not sorted out BILLING ISSUES


au Hawajalipa DENI


Hayo ndo maneno yanayosomeka pindi ukitaka kupata taarifa kutoka katika tovuti ya wizara ya elimu.

Inawezekana kabisa ni ukata kwa wizara au nchi yetu maana hadi hii leo hawajatoa majina ya watu wanaotakiwa kujiunga na course za ualimu katika vyuo vya ualimu nchini.

Vyuo vya ualimu vilifungiwa mitambo mikubwa sana ya internet na ya gharama kubwa lakini hii leo wameshindwa kuwalipia huduma hiyo na vyumba vya ICT vimefungwa vyuo vyote. ICT katika vyuo vya ualimu ilianzishwa kwa mbwembwe kibao lakini vyumba hivyo vanakaribia kufanywa karakana. ISP wanawadai hela kibao.

jamani tuangalie nchi inakoelekea.
 
Hii ni noma,wizara kubwa km hiyo inaingia ktk ukata wa namna hiyo. Nakumbuka kuna kipindi hii ilitokeaga hata kwa wizara ya habari. Hii ndio Tanzania ya Kikwete.!!
 
Wakati mwingine nahisi hela za safari huwa anachukuaga kwenye hizi wizara ndo maana huwa zinashindwaga kufikia malengo zinayojiwekea
Hii ni noma,wizara kubwa km hiyo inaingia ktk ukata wa namna hiyo. Nakumbuka kuna kipindi hii ilitokeaga hata kwa wizara ya habari. Hii ndio Tanzania ya Kikwete.!!
 
Hii nimeikuta kwenye website ya Wizara ya elimu. Na website yao haifunguki ila yanaonekana maandishi yafuatayo

This account has been suspended.

Either the domain has been overused, or the reseller ran out of resources.

or has not sorted out BILLING ISSUES


au Hawajalipa Deni!
 
Halafu ndo wizara mojawapo iliyopo ktk mpango wa BRN. Km haina hela ya kulipia bill ya ku-host tovuti yao,wataweza kweli kutekeleza na kusimamia goals za BRN. Au kuongeza div 5 na zeros ktk shule za kata,kwao ndo BRN..
Wananchi wa kawaida Tanzania tutasubiri sana.
 
inauma sana hasa kwetu tunaoitegemea serikal ktk mambo ya masomo n.k
 
WIZARA MZIGO TU HII, BUDGET YOTE KA TOVUTI WANASHINDWA KULIPIA JE NA WANAVYO SEMA WANATOA MKOPO KWA STASHAHADA YA SCIENCE UALIMU WATATOA KWELI KAMA MAMBO YENYEWE NDO HAYA?
Bora watoe majina hayo pale nacte
 
Mwisho chini kumeandikwa kwa red font color...au hawajalipa deni.
 
TOVUTI YA WIZARA YA ELIMU KULIKONI?

Ni kama wiki nzima sasa tovuti ya Wizara ya elimu Suspended Domain haiko accessible, ikiwa na maandishi yafuatayo;

"This Account has been Suspended.

Either the domain has been overused or reseller ran out of resources.

or has not sorted out BILLING ISSUES.

au hawajalipa DENI"

Jamani seriously taasisi kubwa ya serikali kama hii inafanya mambo kienyeji kama haya? Uko wapi weledi wa viongozi wa wizara? Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kwa utaratibu huu....? My foot!

Wananchi na sisi wadau wa elimu tunahitaji maelezo yasiyo ya longolongo. Je wizara imekosa fedha za kulipia hosting, ISP au kuna sarbotage?
 
Back
Top Bottom