Kwanini Wizara ya elimu inafanya majaribio hatari kwa elimu ya watoto wetu?

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
12,823
Reaction score
21,210
Mwaka 2016 kulitolewa sera na muongozo mpya wa elimu ya msingi.

Mitaala ikabadilishwa na kutolewa maelezo kwamba elumu ya msingi itaishia darasa la 6 badala ya darasa la 7 kama zamani.

Wazazi, wanafunzi na shule wote wakajiandaa na jambo hilo ikiwemo kuhusu plani ya bajeti namna watakavyo somesha watoto wao.

Hii ikimaanisha mzazi aliweka malengo nitamudu gharama za miaka 6 kwa shule zenye gharama hizi na ubora huu.

Mitaala ilibadilishwa ili mtoto aweze kufundishwa yote ya msingi(lazima) ya miaka 7 ndani ya miaka 6.

Kitu cha kushangaza ghafla serikali imekuja na tamko jipya kama nilivyo nukuu toka tovuti ya gazeti la Mwananchi hapo chini.

Wadau naomba tutoe maoni yetu na kuishauri serikali kibidi tukosoe au tupongeze.

Binafsi nimeona hii wizara kila awamu au kila waziri mpya anakuja kuvuruga tu na sio kuendeleza au kuboresha elimu yetu.

-------------------------------------------------------
Serikali yababadili msimamo muda wa kumaliza elimu ya msingi
By Sharon Sauwa, Mwananchi ssauwa@mwananchi.co.tz
IN SUMMARY

Mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi ameibua bungeni utekelezaji wa Sera ya elimu ya msingi kuishia darasa la sita badala ya darasa la saba.
https://mobile.mwananchi.co.tz/Haba...97580-5075672-format-xhtml-iftulgz/index.html
Dodoma. Serikali imesema kwa sasa hakuna haja ya kubadilisha muda wakuhitimu elimu ya msingi kwa sababu imebaini muda wa miaka saba unaotumika si kitu kibaya.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ameyasema hayo leo Jumatano Aprili 17 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi.
Shangazi amehoji Serikali inasemaje kuhusu kutotekelezwa kwa sera ya elimu ya kuishia darasa la sita badala ya darasa la saba.
“Ni lini Serikali itapitia upya sera ya elimu kwa lengo la kuongeza tija na kuendelea na mahitaji ya sasa?…na ni kwa kiasi gani imezingatia ubora wa elimu?,” amehoji.
Akijibu, Ole Nasha amesema sera syio msahafu na kwani Serikali inaweza kuibadilisha wakati wowote kadri itakavyoona inafaa kwa wakati husika.
“Kwa wakati huu tumeona elimu kuanzia darasa la kwanza hadi la saba siyo kitu kibaya. Hatuna haja ya kubadili ndiyo maana tumebakia na mfumo wa zamani,” amesema.
Amesema kwa hatua hiyo Serikali haijavunja sheria na kwa sasa ipo katika mapitio kwa mambo mapya yaliyoko katika sera ya elimu ambayo wanaona hawataweza kutekeleza.
Amesema Serikali inazingatia ubora wa elimu ndiyo maana kumetokea mabadiliko makubwa katika idara ya udhibiti wa elimu.
Amesema wameanza utaratibu mpya wa udhibiti ubora wa elimu kwa ushirikishwaji ambao unawaleta wadau wote kwa pamoja.
Pia wanahakikisha warataibu wa elimu wanapata vifaa na ofisi ili kusimamia vizuri kuhakikisha elimu inakuwa bora.
Amesema Serikali katika utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 imebaini baadhi ya maeneo hayajakaa sawa.
Amesema mchakato wa kupitia upya sera hiyo unaendelea na wakati muafaka ukifika watawashirikisha wabunge.
Mbunge wa Mtambile (CUF), Masoud Abdallah Salim amesema mara kadhaa Serikali imekuwa ikiahidi bungeni kuboresha maslahi ya walimu.
Hata hivyo, amesema wanaopata posho ya kufundishia ni waratibu elimu na wakuu wa shule na kuhoji iwapo Serikali iliwadanganya walimu.
Akijibu, Ole Nasha amesema ni kweli maslahi ya walimu ni muhimu katika kuwaweze kufanya vizuri.
“Serikali inapitia upya maslahi ya watumishi wa umma wote wakiwamo walimu ili tuweze kuwa na maslahi yanayoendana na wakati,” amesema.
Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete amesema muundo wa bodi za shule umeelekeza kutoa nafasi kubwa kwa walimu ambapo wajumbe walimu ni watano na wazazi watatu.
“Je katika dhana nzima ya kwenda kuangalia ufanisi wa elimu, wizara haioni kwamba jambo hili imekosea na linahitaji lirekebishwe kwa haraka sana kabla ya mambo hayajaharibika?, ”amehoji.
Akijibu, Ole Nasha amesema wamegundua maeneo yanayoweza kuwa bora na kwamba Serikali inapitia upya ili kuwa na mwongozo utakaopeleka mbele zaidi elimu.
 
Kinachoshtusha zaidi eti kuanzia Grade 1 mpaka 5 wanatumia Mtaala wa 2016. Wakifika grade 6 na 7 wanatumia old curriculum ya 2005.
Inafaa iwepo Updated curriculum inayoonesha flow ya contents vizuri toka Kindergarten mpaka grade 7.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
elimu ya msingi nchi hii ni majanga sana,na bado lile la kuchukua walimu wa sekondari kuwapeleka kufundisha msingi,watu wanaona poa tu hasa ambao sio waalimu na hawaujui ualimu,kama wangeujua ualimu walahi wasingekubali watoto wao wakafundishwe na walimu wa sekondari.
 
Tatizo letu Sugu wa Tanzania ni pale ambapo tunaamini kua kiongozi ana mawazo mazuri kuliko yoyote yule na chochote atakacho amua lazima tukifuate. Yaani tumekosa taasisi imara zenye sera na miongozo ya kudumu. Taasisi ikiwa imara na kukawa na sera, kanuni na miongozo isiyobadilishwa ovyo ovyo mtu yoyote ye hata mjinga anaweza kua kiongozi. Kwan yy haamui chochote bali kuhakkisha kua watu wanatimiza wajibu wao. Sasa mtu anapokwambia kua mm ndo ntawaletea maendeleo...what shit. Anaweza kuniletea ugali jioni nkala na akanijengea nyumba?

Itazame Uingereza na mchakato wake wa Brexit, hawajataka kukurupuka. Wanafata protocols zote ili wasije wakalaumiana. Ingekua Tz ungeskia tamko tu kua Tz imejiondoa na wote mnapiga makofi. Nchi ya vipofu hii. Udsm pale kuna watu wenye akili na upeo mpana wanaweza kututungia sera na miongozo ya kutumia mda mrefu, sasa hawsna faida yoyte tena wanaimba nyimbo za kuabudu na kusifu. Nchi ya ajabu sana hii. Angalia TCRA wanavokuja kukurupuka tena na alama za vidole. Utadhan hawajaenda shule. Hawajui madhara yake. Hata mke wangu alieishia darada la saba walipotangaza tu akabainisha madhara yake ila wao hawajui.

Tassisi za serikali hazuna mfumo "main center" ambako wote wangeenda kukutana. NIDA tayali wana alama za vidole za watu, ya nn tena udai alama za vidole na tayali watu washajisajili?
Utamzuia jambazi kutumia simu? Utamzuia mnyarwanda kua na lain? Mbona vitambulisho na vyeti vya kuzaliwa mshawapa tayali?
 
Mwaka 2016 kulitolewa sera na muongozo mpya wa elimu ya msingi.

Mitaala ikabadilishwa na kutolewa maelezo kwamba elumu ya msingi itaishia darasa la 6 badala ya darasa la 7 kama zamani.

Wazazi, wanafunzi na shule wote wakajiandaa na jambo hilo ikiwemo kuhusu plani ya bajeti namna watakavyo somesha watoto wao.

Hii ikimaanisha mzazi aliweka malengo nitamudu gharama za miaka 6 kwa shule zenye gharama hizi na ubora huu.

Mitaala ilibadilishwa ili mtoto aweze kufundishwa yote ya msingi(lazima) ya miaka 7 ndani ya miaka 6.

Kitu cha kushangaza ghafla serikali imekuja na tamko jipya kama nilivyo nukuu toka tovuti ya gazeti la Mwananchi hapo chini.

Wadau naomba tutoe maoni yetu na kuishauri serikali kibidi tukosoe au tupongeze.

Binafsi nimeona hii wizara kila awamu au kila waziri mpya anakuja kuvuruga tu na sio kuendeleza au kuboresha elimu yetu.

-------------------------------------------------------
Serikali yababadili msimamo muda wa kumaliza elimu ya msingi
By Sharon Sauwa, Mwananchi ssauwa@mwananchi.co.tz
IN SUMMARY

Mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi ameibua bungeni utekelezaji wa Sera ya elimu ya msingi kuishia darasa la sita badala ya darasa la saba.
https://mobile.mwananchi.co.tz/Haba...97580-5075672-format-xhtml-iftulgz/index.html
Dodoma. Serikali imesema kwa sasa hakuna haja ya kubadilisha muda wakuhitimu elimu ya msingi kwa sababu imebaini muda wa miaka saba unaotumika si kitu kibaya.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ameyasema hayo leo Jumatano Aprili 17 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi.
Shangazi amehoji Serikali inasemaje kuhusu kutotekelezwa kwa sera ya elimu ya kuishia darasa la sita badala ya darasa la saba.
“Ni lini Serikali itapitia upya sera ya elimu kwa lengo la kuongeza tija na kuendelea na mahitaji ya sasa?…na ni kwa kiasi gani imezingatia ubora wa elimu?,” amehoji.
Akijibu, Ole Nasha amesema sera syio msahafu na kwani Serikali inaweza kuibadilisha wakati wowote kadri itakavyoona inafaa kwa wakati husika.
“Kwa wakati huu tumeona elimu kuanzia darasa la kwanza hadi la saba siyo kitu kibaya. Hatuna haja ya kubadili ndiyo maana tumebakia na mfumo wa zamani,” amesema.
Amesema kwa hatua hiyo Serikali haijavunja sheria na kwa sasa ipo katika mapitio kwa mambo mapya yaliyoko katika sera ya elimu ambayo wanaona hawataweza kutekeleza.
Amesema Serikali inazingatia ubora wa elimu ndiyo maana kumetokea mabadiliko makubwa katika idara ya udhibiti wa elimu.
Amesema wameanza utaratibu mpya wa udhibiti ubora wa elimu kwa ushirikishwaji ambao unawaleta wadau wote kwa pamoja.
Pia wanahakikisha warataibu wa elimu wanapata vifaa na ofisi ili kusimamia vizuri kuhakikisha elimu inakuwa bora.
Amesema Serikali katika utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 imebaini baadhi ya maeneo hayajakaa sawa.
Amesema mchakato wa kupitia upya sera hiyo unaendelea na wakati muafaka ukifika watawashirikisha wabunge.
Mbunge wa Mtambile (CUF), Masoud Abdallah Salim amesema mara kadhaa Serikali imekuwa ikiahidi bungeni kuboresha maslahi ya walimu.
Hata hivyo, amesema wanaopata posho ya kufundishia ni waratibu elimu na wakuu wa shule na kuhoji iwapo Serikali iliwadanganya walimu.
Akijibu, Ole Nasha amesema ni kweli maslahi ya walimu ni muhimu katika kuwaweze kufanya vizuri.
“Serikali inapitia upya maslahi ya watumishi wa umma wote wakiwamo walimu ili tuweze kuwa na maslahi yanayoendana na wakati,” amesema.
Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete amesema muundo wa bodi za shule umeelekeza kutoa nafasi kubwa kwa walimu ambapo wajumbe walimu ni watano na wazazi watatu.
“Je katika dhana nzima ya kwenda kuangalia ufanisi wa elimu, wizara haioni kwamba jambo hili imekosea na linahitaji lirekebishwe kwa haraka sana kabla ya mambo hayajaharibika?, ”amehoji.
Akijibu, Ole Nasha amesema wamegundua maeneo yanayoweza kuwa bora na kwamba Serikali inapitia upya ili kuwa na mwongozo utakaopeleka mbele zaidi elimu.
Ulitegemea wafanyie wapi kama hatujitambui power yetu imeshikiriwa
 
Back
Top Bottom