Kwanini Xavier Hernández Creus(42) Hana mpango na Frenchie De Jong?

Kwanini Xavier Hernández Creus(42) Hana mpango na Frenchie De Jong?

Cheology

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2022
Posts
384
Reaction score
601
Kama heading inavyo

Xavier Hernández Creus almaarufu Xavier kiungo mstaafu na kocha wa Barca huyu fundi ni kwanini anaonekana kumchukia fundi Frenchie De Jong!

Nikiwa mdau wa mashetani The Red devils nimekuwa nikifuatilia Sana usajili wake Kwa man utd, na wakati yeye anaipenda Barca, kocha Hana mpango Naye japo akiulizwa anadanganya kuwa yupo kwenye mipango yake. Hivi karibuni Kwa Siri sana anaonekana kumhiraji mshambuliaji Kwa gharama za Frenchie De jong.

Binafsi nikaanza kumuona de jong mzinguaji. Cha ajabu majuzi fundi huyu mdachi anaona Sasa kuwa hahitajiki.

Swali Kwa mafundi watambuzinwa soka, huyu fundi Xavier Hernández Creus Kwa nini hamkubali fundi mwenzie?
 
Huenda kuna vitu anakosa, hivyo hatofaa kwa mbinu za xavi..

Ni wachezaji wachache saana ambao wanaweza kucheza kwa kila mwalimu.
 
Katika kumfuatilia kwangu mwandishi gwiji wa habari za usajili, Fabrizio Romano ni kwamba, rais wa Barcelona, Joan Laporta na De Jong mwenyewe wanapenda kuendelea kuwa hapo Nou Camp,

Lakini Xavi anamuona dogo huyo hafiti kwenye mfumo wake kwa sababu, yeye ni mtu wa mpira wa nguvu sana badala ya ile total football.

Ndio maana anataka kutumia thamani yake kubwa sokoni ili apate mshambuliaji mzuri atakayefifi kwenye mbinu zake.

De Jong akitua Manchester United atawasaidia, kwa sabahu soka la nguvu la England analimudu kutokana na aina yake ya uchezaji wake.

Lakini yeye mwenyewe hataki kwenda Man United kwa sababu moja tu, hawapo Ligi ya mabingwa Ulaya, halafu mke wake haipendi nchi ya England kwa sababu ya hali ya hewa na tayari kanunua jumba la thamani pale Katalunya
 
Kwanini iwe kwa de jong na sio yule mbrazili!!! Ana faida gani katika timu huyu mbrazili!! C mwingine ni dani alves. Angelikua pep asingeruhusu huu ujinga, sometimes ushkaji ukae pending, azawaiz unaigharimu timu.
 
[emoji38]
Screenshot_20220712-214852.jpg
 
Back
Top Bottom