Kwanini Yanga na Singida wapo kambi moja Tanga?

Dabil

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2021
Posts
6,823
Reaction score
15,293
Wakati Ngao ya jamii inaanza Yanga Singida walikuwa kambi moja na kufanya mazoezi pamoja.

Hii ni match fixing kama zingine tu. Je, kwenye ligi wanapokutana lazima Singida waachie, ndo maana mechi ya Yanga na Singida lazima Yanga washinde.

Nakumbuka msimu uliopita Singida walifungwa na Yanga halafu wakapost, sisi tumefungwa na Yanga kwanini wengine waumie.

Msimu huu tusitegemee mechi ya ushindani kati ya hawa ndugu wa tumbo moja.
 
Ongeeni na Azam vizuri ni kama ameanza kuwasaliti ila Karia mtaalamu sana kahakikisha msimu huu mnapata medal
 
huo ni mpango wa mazoezi kwa usimamizi wa tff kwakuwa tanga hakuna viwanja
 
Malalamiko mengi kama watoto wa kambo Yanga wapo Mountain usambara hotel, Singida wapo Sea view hotel muwe mnafatilia vitu kabla ya kupost

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Kumbe ndio maana siku ya mechi ya Simba vs SFG Yanga walikuwa wanashangilia sana Simba ilipokuwa inashambuliwa.

Mechi ilivyoisha bila kufungana wakaungana Yanga na SFG kushangilia wakiamini Beno atawavusha kwenye penati kuliko Salim wakisahau Luis pia anatumiaga mguu wa kulia.

Baada ya matokeo Yanga ndio wameumia zaidi baada ya kugundua sasa watakutana ana kwa ana na dude la kutisha Simba sc
 
Sio Yanga tu hata Azam wote wanatumia uwanja 1 kufanya mazoezi sema yanatofautishwa mda tu.
 
Fwatilia ukweli maana hapa umejaza hisia tu
Yanga ,singida ,Azam na hata Simba Leo wametumia uwanja moja kufanya mazoezi kinachotofautiana ni masaa tu na ndo maana hata Leo kipindi Yanga wanaondoka uwanjani kufanya mazoezi Simba ndo walikua wanaingia.
 
Kumbe ndivyo ulivyoona. Vipi wachezaji wa Simba waliokuwa uwanjani kuangalia mechi kati ya Yanga dhidi ya Azam, ilikuwaje baada ya Yanga kufunga goli wakainuka na kuondoka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…