Kwanini Yesu aliyaelekeza mapepo kwenda kwa Nguruwe na si mnyama mwengine?

Kwanini Yesu aliyaelekeza mapepo kwenda kwa Nguruwe na si mnyama mwengine?

Mfupawasokwe

Member
Joined
Sep 12, 2024
Posts
24
Reaction score
29
Habari yenu, kama kichwa cha habari kinavyojieleza kwanini yesu alipokuwa anaombea watu wenye mapepo alikua anayotoa hayo mapepo kwa watu na kuyaelekeza kwa nguruwe, naomba msaada mnieleweshe maana hili linanichanganya.
 
Kwa sababu walikuwa haramu (najisi) kwa mujibu wa sheria ya torati...
 
Wale nguruwe walikua wa Wagerasi kina Maghayo Stress Challenger nk
Sasa unajua Israelites hawali my wetu haram kama kina adriz
Hivyo kutokana na coincidence wale jamaa walikua wanachungwa lile eneo yaani zamani nguruwe walichungwa kama mbuzi na ng'ombe 😁
Yesu akaona isiwe tabu kuliko mtu afe bora mwanahamu ngubi yifwile ku lulenga!
😁😁😁
 
Kwa sababu watu wa eneo lile ulikuwa uwaambii kitu kuhusu nguruwe wao. Yaani utajiri na heshima yao na kiburi chao kilikuwa juu ya kumliki nguruwe wengi. Hivyo Yesu alitaka kuwapa fundisho kwamba hicho mnacholingia kwenye mwili wa nyama kinaweza kugeuzwa kikawa takataka na hivyo kisikufae abadani. Ndoo maana Yesu baada ya kuelekeza pepo wale kwa wale nguruwe wote waliongozana kuelekea mtoni na kufia huko.
Ujumbe huo wa Yesu, kwetu sisi wanadamu wa leo tusitukuze mali tulizanazo na kujiona sisi ni wajanja tuliojawa viburi maana kwa mali hizo ulizojilimbikizia zinaweza kuwa tiketi yako kuingia motoni.
 
Sasa kwanini baadhi ya madhehebu ya kikristo wanakula hali ya kuwa huyo mnyama ni haramu.
Hata kama wasinge kula dhambi ni zaidi ya NAJISI mtu akila nguruwe atakiwi kutubu bali anachotakiwa kufanya ni kutawaza na anakuwa safi...vipo vitu avifai ila siyo dhambi bali vina halibu dhawabu au vinazuia dhawabu au vinazuia kusikiwa na mungu kwenye dua zako ...ndiyo maana unajisi wa nguruwe haupo kwenye kumla tu kama wengi mnavyo dhani bali hata kugusana naye ...swali je .. watu wa torati wakiwa wanakwenda hekaluni kisha nguruwe akawapitia na kuwagusa bija ya dhamira zao walinajisika hau la ? Bila shaka walinajisika ...je kuna dhambi yoyote inayoweza kumpata mtu bila ya yeye mwenyewe kukusudia moyoni? Jibu hapana .. hivyo kitu najisi ni chochote ambacho mungu akihesabii dhambi ila kina zuia kusikiwa na mungu... hata kumwomba mungu ukiwa umekunywa pombe ni najisi ...kwanini sababu ni kuwa mungu awezi kukusikia dua zako..zamani mitume na watakatifu wengi tu walikuwa wanakunya pombe .
Tofsuti ya dhambi na najisi ni swana na
DHAMBI =UHALIFU
NAJISI =KUKOSEA
Mfano wa najisi kwa waislamu ni kama kujamba msikitini ni NAJISI ila siyo dhambi...kama muislamu akijamba msikitini basi dua zake aziwezi kusikiwa hivyo ulazimika kujitakasa kwa kutawaza tena
 
Habari yenu, kama kichwa cha habari kinavyojieleza kwanini yesu alipokuwa anaombea watu wenye mapepo alikua anayotoa hayo mapepo kwa watu na kuyaelekeza kwa nguruwe, naomba msaada mnieleweshe maana hili linanichanganya.
Kwa sababu eneo hilo hakukuwa na wanyama wengine isipokuwa hao nguruwe.
 
Habari yenu, kama kichwa cha habari kinavyojieleza kwanini yesu alipokuwa anaombea watu wenye mapepo alikua anayotoa hayo mapepo kwa watu na kuyaelekeza kwa nguruwe, naomba msaada mnieleweshe maana hili linanichanganya.
Yesu hakuelekeza, mapepo yalipendekeza
 
Habari yenu, kama kichwa cha habari kinavyojieleza kwanini yesu alipokuwa anaombea watu wenye mapepo alikua anayotoa hayo mapepo kwa watu na kuyaelekeza kwa nguruwe, naomba msaada mnieleweshe maana hili linanichanganya.
Kuna kitu hakipo sawa ulivyoandika.Kwamba Yesu kila alipowatoa watu mapepo(zingatia neno kila)aliamuru waemde kwa nguruwe?Kasome upya biblia yako ya kiwapi sijui!
 
Back
Top Bottom