Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Yesu Kristo alipokuja duniani alifanya mambo mengi ambayo hayaruhusiwi kufanywa siku ya Sabato. Kwa mfano, aliwaponya wagonjwa na pia aliwaruhusu wanafunzi wake wavunje masuke ya nafaka siku ya Sabato.
Hiyo ilikuwa kinyume na sheria ya Sabato. Wakati wa Musa, Mungu aliwaagiza Wana wa Israeli wapumzike siku ya saba ili kukumbuka jinsi walivyokuwa watumwa katika nchi ya Misri na jinsi BWANA Mungu alivyowatoa utumwani na kuwapa pumziko(Kutoka 20:8-11)
Yesu Kristo alipokuja alisema hakuja kuitangua torati bali kuitimiza. Kama ni hivyo, kwanini sasa kuna Maandiko mengi yanayoonyesha kuwa Yesu aliivunja Sabato? Ni kwanini Yesu aliivunja Sabato badala ya kuitimiza?
Iko hivi: Kabla ya kuja kwa Yesu, Nabii Hosea alitabiri kuwa Mungu ataikomesha Sabato (Hosea 2:11). Yesu Kristo ni Mungu, alipokuja aliikomesha Sabato. Ndio sababu Yesu alifanya mambo hayo yaliyopingana na sheria ya Sabato. Yesu alisema Yeye ndiye Bwana wa Sabato. Kwa kuwa Yesu Kristo ni Bwana na aliivunja Sabato, ndiyo sababu Wakristo nao wanaona ni halali kuivunja sabato kwa kuwa Yesu amewaachia kielelezo wafuate nyayo zake (Kol 2:13-14).
Mtume Paulo anaeleza pia kwamba kushika siku na miezi na nyakati na miaka ni kuyarejea mafundisho manyonge yenye upungufu (Gal 4:9-11).
Je, umewahi kujiuliza kwanini katika zile amri kumi, amri ya nne(ya sabato) haipo katika Agano Jipya? Sababu kuu ni hiyo kwamba Yesu aliye Bwana wa Sabato aliikomesha sabato kama ilivyokuwa imetabiriwa ili watu wapate pumziko la kweli kwa kumwendea Yesu, wanaposumbuka na kulemewa na mizigo (Mt 11:28).
Wote wanaokaa ndani ya Yesu wanapumzishwa hapa duniani, na pia watapumzika katika Sabato ya milele mbinguni (Ebr 4:8-11). Fanya bidii uwe miongoni mwa watu hao watakaoingia katika raha hiyo ya milele. Wanaotenda dhambi hawataingia (Ebr 4:1-11; Ufu 14:13).
Kwakuwa Yesu aliivunja Sabato, ndio sababu Wakristo wanasali au kuabudu siku ya Jumapili ambayo ni siku ya kwanza ya juma. Kwa Wakristo:
Kwaya na Wasanii wa Nyimbo za Injili, siku ya Jumapili wanaimba nyimbo tamu lakini wakitoka kanisani wanasengenya watu, wanasema uongo, na wengine wanafanya uzinzi na kulewa pombe. Nyimbo zinazoimbwa Jumapili na watu wa aina hiyo ni kelele mbele za Bwana. Soma uzi huu hapa 👇 upate ufahamu wa kina kwa nini Mungu anaziita nyimbo “kelele”
www.jamiiforums.com

- Jumapili ni siku ya ushindi, kwa sababu ndiyo siku ambayo Yesu Kristo alifufuka
- Ni siku aliyokuja Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu alikuja siku ya Jumapili - siku ya Pentekoste (Mdo 2:1).
- Jumapili ndiyo siku ambayo kanisa la kwanza lilianza kuhubiri na watu 3,000 wakaokoka na kuanza kukusanyika pamoja katika ibada (Mdo 2; 20:6-12; 1Kor 16:1-2).
Kwaya na Wasanii wa Nyimbo za Injili, siku ya Jumapili wanaimba nyimbo tamu lakini wakitoka kanisani wanasengenya watu, wanasema uongo, na wengine wanafanya uzinzi na kulewa pombe. Nyimbo zinazoimbwa Jumapili na watu wa aina hiyo ni kelele mbele za Bwana. Soma uzi huu hapa 👇 upate ufahamu wa kina kwa nini Mungu anaziita nyimbo “kelele”
Wasanii wa nyimbo za Injili acheni kumpigia Mungu kelele
Naongea na nyinyi mnaojiita wasanii wa nyimbo za Injili (Gospel Artists), vikundi vya kwaya na bendi. Nyinyi mnaotunga na kuimba nyimbo za Injili, nyimbo za sifa na kuabudu lakini maisha yenu ni ya mchanganyo! Maisha ya uvuguvugu. Nyinyi mnaopenda kumwimbia Mungu lakini dhambi hamtaki kuziacha...