kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Kesi nyingi za uhujumu uchumi Tanzania utasikia uchunguzi haujakamilika, na hii inachukua miaka kadhaa. Ila katika mazingira ya uchunguzi kuendelea mtu yuleyule unasikia ameshauriana na DPP au Mahakama na ameeelekzwa kulipa kiasi flani Cha fedha.
Je, ukokotoaji wa kiasi hicho kinacholipwa unafanywa na Nani?
Hakuna uwezekano uchunguzi ungekamilika zingekuwa fedha nyingi zaidi?
Kwanini hakuna uchunguzi zaidi unaoendelea baada ya mazungumzo?
Wachunguzi awaoni kwamba walipaswa kuendelea na uchunguzi hata baada majadiliano?
Kwanini tunaamini uchunguzi wa uhujumu uchumi unapaswa kutokamilika ila watuhumiwa hawastahili dhamana?
Je, Kama wanachodaiwa ni fedha, kwanini wasipewe dhamana wakazitafute hizo fedha? Maana dhamana inakatazwa kwa wale watu ambao maisha yao yanaweza kuwa hatarini uraiani lakini kumweka mtu ndani kisa unataka fedha sioni kama ina tija.
Tanzania ni moja, kwanini huu utaratibu Zanzibar haupo?