G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 12,505
- 40,002
Kiini macho na kihoja kuliko vyote ndani ya nchi ya Zanzibar ni kuwa miaka 56 iliyopita tarehe kama ya leo walipata uhuru wao kutoka kwa mkoloni Muingereza. Sijui ni kutokana na mila walizowekewa na yule anayeandaliwa kuwa mwenye heri ila hawajawahi kuadhimisha siku hii.
Mwezi mmoja baadaye ASP wakaipindua serikali iliyowapatia wazanzibar uhuru na wao wakajitwalia madaraka na ndicho wanachosherehekea hadi leo. Wanakiita mapinduzi matukufu.
Halafu tulikuwa tunaaminishwa kuwa Sultani aliyeitawala Zanzibar alikuwa dhalimu. Udhalimu gani alioufanya ndani ya mwezi mmoja tangia apate uhuru?
Mkuu Mohamed Said hebu tusaidie kwanza ni kwanini nyie wazanziberi hamuadhimishi siku ya uhuru wenu mlioupata tarehe 10 December 1963? Kwanini muadhimishe mapinduzi ambayo mpaka leo hayajulikani hasa lengo lake la halali? Pascal Mayalla unaweza pia kutusaidia
Bendera ya Zanzibar ambayo ilipandishwa baada ya uhuru